NONDO NNE ZA: MAYWEATHER V MCGREGOR

NONDO NNE ZA: MAYWEATHER V MCGREGOR

463
0
KUSHIRIKI

 

LAS VEGAS, Marekani


 

BAADA ya bondia Floyd Mayweather na Conor McGregor kutambiana kwenye mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita, sasa wakali hao wamerudi ‘gym’ kuendelea na mazoezi kabla ya pambano lao litakalopigwa Agosti 26, mwaka huu.

Ukiachana na fujo, utani na kejeli walizotoleana wakali hao wakiwa kwenye miji ya Los Angeles, Toronto, New York na London, kuna maeneo manne unayotakiwa kuyafahamu na kuyaelewa kuhusu pambano hilo linalovuta hisia za wadau wengi wa michezo duniani.

 

1.Vita ya kisaikolojia

Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, Mayweather kwa sasa ana wasiwasi sana na mienendo ya mpinzani wake kuanza kumvuruga kiakili.

McGregor ameshazoea kuwavuruga wenzake kama ilivyotokea kabla ya mapambano dhidi ya Jose Aldo na Eddie Alvarez. Na sasa anajaribu kadiri ya uwezo wake kukitikisa kichwa cha Mayweather kwa kuzungumzia matukio yake ya ugomvi na kifedha wakiwa kwenye mikutano na waandishi wa habari.

 

2.Watafaidika kibiashara

Wote wawili watafaidika sana kwenye malipo na biashara; Mayweather atapata promosheni ya kutosha ya bidhaa zake zikiwamo nguo na kofia huku McGregor akipata faida ya matangazo ya kampuni yake ya michezo na burudani.

Zaidi itakuwa ni kwa McGregor ambaye kampuni yake hiyo haijatimiza mwaka mmoja.

 

3.Hakuna wa kufika raundi ya 12

McGregor aliahidi kuwa mpinzani wake hatofika raundi ya nne, ni ahadi inayoonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kutimia, lakini kuna dalili zote kuwa pambano hilo halitofika raundi nyingi.

Katika udhaifu ambao McGregor anaufahamu juu yake ni kwamba, huwa anapungua makali kadiri raundi zinapozidi kuongezeka, hivyo hataona shida kujiachia raundi za kwanza ili mpinzani wake naye afunguke, hapo mmojawapo lazima ataangushwa kabla hatujaanza kufikiria kuwa huenda mshindi akapatikana kwa pointi.

 

4.Wengi watamsapoti McGregor

Kwa sasa wengi hawamkubali Mayweather tangu alipoutia aibu mchezo wa masumbwi kwa mbinu zake za kujilinda dhidi ya Manny Pacquiao.

Asilimia kubwa ya wadau hao wanadhani bondia huyo hatafurukuta mbele ya McGregor.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU