PENGO LA SIMON MSUVA LAMTESA CANNAVARO

PENGO LA SIMON MSUVA LAMTESA CANNAVARO

3674
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI


WINGA wa Yanga, Simon Msuva, ameonekana kumuumiza kichwa nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro,’ baada ya kusema wazi kwamba itachukua muda kuziba pengo lake.

Msuva anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo Alhamisi wiki hii kwenda kujiunga na Klabu ya DIfaa El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Akizungumza na BINGWA jana, Cannavaro alisema kuondoka kwa Msuva katika kipindi hiki, ni jambo ambalo litachukua muda kusahaulika kwa mchezaji huyo katika nafasi anayocheza.

Cannavaro  alisema mchango wa Msuva katika klabu hiyo ni mkubwa na Yanga bado inamhitaji,  lakini hakuna jinsi  ni wakati wake wa kwenda  kuendeleza kipaji chake na kupata changamoto nyingine.

Alisema haitakuwa rahisi kupata mchezaji wa aina yake kwa haraka, itachukua muda mrefu hadi kupatikana mtu atakayeendana na uchezaji wake na jina lake kuondoka midomoni mwa Wanayanga.

“Msuva ni mchezaji tunayemtegemea sana kwenye klabu ya Yanga kutokana na mchango wake na kujituma uwanjani.

Kiwango chake kwa sasa kipo juu muache tu aende ila kwa maoni yangu mimi, itachukua muda sana kumpata mbadala wake kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine,” alisema Cannavaro.

Alisema alikuwa anampenda kutokana na ushirikiano wake ndani na nje ya uwanja katika  kuhakikisha klabu yake inapata mafanikio.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU