RAPA DMX JELA MIAKA 44 KWA UKWEPAJI KODI

RAPA DMX JELA MIAKA 44 KWA UKWEPAJI KODI

525
0
KUSHIRIKI

NEW YORK, Marekani


RAPA wa Marekani, DMX, kwa sasa ameingia kwenye matatizo na Serikali ya nchi hiyo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kukwepa kodi kiasi cha dola milioni 1.7.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa rapa huyo alikuwa akificha mapato yake kwa miaka kadhaa.

DMX alitajwa kukwepa kutumia akaunti zake binafsi na kutumia zile mbadala.

Rapa huyo pia alilipwa kiasi cha dola 125,000 kwa kuibuka katika kipindi cha televisheni cha ‘Couples Therapy’, lakini alipoletewa ‘cheki’ iliyoelezea kwamba ameshakatwa kodi, akaomba iliyo na kiasi kamili na akapewa.

Taarifa hizo ziliorodhesha pia kuwa mwaka 2011 na 2012 alipokea kiasi cha dola 353,000 na 542,000.

Mwaka 2013, aliripoti kupokea kiasi cha dola 10,000 japokuwa ukweli ni kwamba mwaka huo alipokea kiasi cha dola 250,000.

Aidha, mtandao wa TMZ uliripoti kuwa DMX alijitokeza mwenyewe mbele ya vyombo vya dola juzi Julai 13 na kama atakutwa na hatia ya kukwepa kodi kwenye akaunti 14, huenda akaswekwa rumande kwa muda wa miaka 44.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU