SINGANO AMUWAHI MSUVA MOROCCO

SINGANO AMUWAHI MSUVA MOROCCO

2550
0
KUSHIRIKI

NA ZAITUNI KIBWANA


KIUNGO mshambuliaji wa Azam, Ramadhani Singano ‘Messi’, amemuwahi mwenzake Simon Msuva baada ya kuondoka nchini juzi kujiunga na klabu ya Difaa Hassani d’ El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Messi ambaye mkataba wake umemalizika hivi karibuni na klabu yake ya Azam, amekwenda nchini Morocco kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo yenye timu 16.

Wakati Messi akiondoka nchini, winga wa Yanga, Simon Msuva ambaye naye anapigiwa hesabu na klabu hiyo, anatarajia kuondoka nchini Alhamisi hii ili kujiunga na klabu hiyo.

BINGWA lilimtafuta Meneja wa Azam, Philiph Alando, kuzungumzia safari ya winga huyo ambapo alisema kuwa klabu hiyo haina taarifa na lolote lile kwa kuwa walimalizana naye toka mkataba wake umalizike.

“Mkataba wa Singano ulikuwa umemalizika Julai 8, mwaka huu hivyo sisi hatuna mazungumzo naye yoyote na wala hatujui kuhusu hiyo safari yake ya Morocco wala chochote kinachoendelea,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU