JAY Z JEURI ILE MBAYA

JAY Z JEURI ILE MBAYA

549
0
KUSHIRIKI

 LOS ANGELES, Marekani

STAA wa hip hop, Jay Z, ameonyesha jeuri yake ya fedha baada ya kuajiri wafanyakazi sita watakaokuwa wakiwahudumia watoto wake wawili waliozaliwa hivi karibuni.

Kama hiyo haitoshi, kwa kazi hiyo tu ya kuwaangalia Rumi na Sir Carter, kila mmoja atakuwa akilipwa kitita cha Dola za Marekani 100,000.

Chanzo kimoja kililiambia jarida la Magazine US: “Mapacha hao hawalali kwa wakati mmoja, hivyo Beyonce alihitaji wafanyakazi watatu kwa kila mmoja, watakuwa wakipeana zamu kila baada ya saa nane.

Itakumbukwa kuwa idadi ya wafanyakazi wa watoto sasa inafika nane baada ya wale wawili ambao wamekuwa wakiishi nyumbani kwa mwanamuziki huyo kwa ajili ya ‘dogo’ Blue Ivy.

Jay Z na mkewe Beyonce wamekuwa wakiishi kwenye mjengo wa kupanga uliopo mjini Malibu, lakini siku chache zijazo watahamia kwenye jumba lao la kifahari lililopo Los Angeles.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU