NGASSA SI BURE, ANA ‘KIZIZI’

NGASSA SI BURE, ANA ‘KIZIZI’

3468
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

Ngassa aliondoka na kijiji cha mashabiki wa klabu hiyo, wakati timu yao ilipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 3-2, baadhi ya mashabiki  walionekana wakilizunguka gari la winga huyo huku wakimsihi arejee Jangwani.

Mashabiki hao walikuwa wakisukuma gari ya Ngassa na kuimba nyimbo tofauti huku wakimwambia bado  wanahitaji kumuona akikipiga Yanga kwa mara nyingine.

“Ngassa rudi jembe si umeona mwenyewe bado tunakuhitaji, Mbeya City unafanya nini wewe kwako ni  Jangwani, si umeona mwenyewe kila mtu anakushangilia,” walisikika mashabiki hao.

Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa Wanajangwani hao kumshangilia Ngassa kila anapojitokeza katika mechi za Yanga  kwani hata alipokuwa Free State ya Afrika Kusini hali ilikuwa hivyo anaporudi Bongo.

Wakati Yanga walipokuwa wanajiandaa na mashindano ya Sportpesa, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wa timu hiyo na alitakiwa kucheza michuano hiyo, kitendo kilichowafurahisha mashabiki wa klabu hiyo, lakini dakika za mwisho aliondolewa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU