DONDOO ZA ULAYA; GUARDIOLA AIVAMIA ARSENAL KWA LEMAR

DONDOO ZA ULAYA; GUARDIOLA AIVAMIA ARSENAL KWA LEMAR

644
0
KUSHIRIKI

Guardiola aivamia Arsenal kwa Lemar

LONDON, England

KOCHA Pep Guardiola ameingia kwenye vita nyingine na Arsenal kwa kuitaka huduma ya kiungo wa Monaco, Thomas Lemar.

Guardiola anamfukuzia Alexis Sanchez, hivyo kumtaka Lemar ni vita ya wazi kwa Arsenal, ambao wamekuwa wakimtolea jicho kwa muda kirefu.

Madrid wadai Bale hang’oki

MADRID, Hispania

REAL Madrid wameshikilia msimamo wao wa kutomuuza Gareth Bale kwa timu yoyote inayotaka kumsajili.

Uongozi wa klabu hiyo umesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ni staa wa baadaye kwenye kikosi hicho.

Chelsea hawamwachi beki wa Southampton

LONDON, England

CHELSEA wameendelea kujipa matumaini ya kumchukua beki wa kati wa Southampton, Virgil van Dijk.

Blues wanaamini wataipiku Liverpool ambayo imekuwa ikimfukuzia Mholanzi huyo kwa udi na uvumba tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili.

 

Dortmund hawahofii kumpoteza Dembele

MUNICH, Ujerumani

WAPINZANI wakubwa wa Bayern Munich, Borussia Dortmund, wameweka wazi kuwa hawatilii shaka uwezekano wa kumbakiza staa wao, Ousmane Dembele.

Kocha wa timu hiyo, Peter Bosz, amesema Mfaransa huyo atabaki Dortmund ingawa anawindwa na klabu vigogo Ulaya.

Barca wamtaka kiungo Ufaransa

CATALUNYA, Hispania

BARCELONA wametangaza kuitaka kwa udi na uvumba saini ya kiungo wa Nice na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Jean-Michael Seri.

Seri, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa maarufu kwenye soko la usajili, ambapo anatakiwa pia na mabosi wa Arsenal.

Liver wafunga rasmi usajili

MERSEYSIDE, England

KWA mujibu wa kocha Jurgen Klopp, mashabiki wa Liverpool wasitarajie kuona mchezaji mpya akiingia kikosini kwani tayari ameshamaliza usajli.

Klopp amedai kuifunga Atletico Bilbao mabao 3-1 ni ushahidi mzuri wa kikosi kizuri alichonacho licha ya kutumia fedha kiduchu.

Jembe Juventus latua England

LONDON, England

KITUO cha televisheni cha Sky Sport, kimenyetisha kuwa Juventus wamempoteza kiungo wao, Mario Lemina ambaye amekubali kutua Southampton.

Nyota huyo wa kimataifa wa Gabon, anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo na Southampton wametumia pauni milioni 16 kumnasa.

Mourinho aahidi kumsajili Roberto

MANCHETER, England

HUKU Chelsea nao wakikazania kumsajili kiungo huyo, kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amewaambia mashabiki wake kuwa watulie kwani atampeleka Old Trafford.

Mchezaji huyo raia wa Hispania, anaichezea Barcelona na msimu uliopita aliichezea mechi 47.

Everton wamvaa Danny Welbeck

MERSEYSIDE, England

EVERTON wameanzisha mpango wa kumsajili straika wa kimataifa wa England, Danny Welbeck.

Mpango huo ni endapo watashindwa kuinasa huduma ya mkali wa mabao, Olivier Giroud ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU