HUYU HAKUPENDI ILA ANATAFUTA KICHAKA CHA KUJIFICHA, MWANGALIE KWA MAKINI

HUYU HAKUPENDI ILA ANATAFUTA KICHAKA CHA KUJIFICHA, MWANGALIE KWA MAKINI

354
0
KUSHIRIKI

MAPENZI hayaumizi bali kinachoumiza ni uongo na usaliti unaofanywa na baadhi ya watu katika mapenzi. Mateso waliyonayo wengi walio katika mapenzi hayasababishi na wao kuthamini na kujali mapenzi, bali ni kwa kuwa wameangukia kwa wapenzi waongo, wasaliti na wasiojua nini thamani halisi ya mapenzi na kupendwa.

Hakuna mtu anayetaka kuumia katika mapenzi. Kila mmoja anataka kuwa katika mahusiano ya raha na amani. Ila wengi hawayapati. Tatizo nini?

Sababu za yote hayo ziko nyingi. Ila kwa leo naomba tujadili moja kwa pamoja.

Bila kuzunguka sana, ni vizuri ikaeleweka kuwa si vyema kumlazimisha mtu akupende kwa upole, pesa, umaarufu au kipaji chako. Mapenzi hayako hivyo.

Mapenzi huja na kitu ambacho mara nyingi ni ngumu kusema kuwa ni kwanini unampenda fulani.

Tabia na vitu vingine huwa vinaongeza raha tu ya mapenzi ila huwa si sababu ya msingi sana ya kumpenda mtu. Mapenzi ni kitu ‘special’. Kitu kigumu kuelezwa kwa maneno na msikilizaji akajua namna halisi ya mhusika anavyojihisi.

Ukiwa mmoja wa watu waliowahi kupenda kwa dhati kuna kitu kinaweza kuwa si kigeni katika fikra zako. Hisia zako zinapoangukia kwa mtu f’lani karibu kila kitu kuhusu yeye huwa unakiona cha kipekee. Kila kitendo chake kinakuwa na maana kubwa kwako.

Anapotazama mahala ulipo unajua aanakuangalia wewe hata kama si mara zote. Ukiongea, akicheka hujihisi faraja au kudharaulika. Ilimradi tu. Mapenzi huleta kitu kigumu sana kuelezeka ndani ya nafsi. Hapa sasa kuna kitu nataka tuongee.

Mara kwa mara nimewahi kushuhudia mtu akimpenda mtu anayempenda mtu mwingine. Na wewe pia unaweza kuwa ni mhanga mmoja wapo. Katika hali hii wengi huwa si wepesi kukubali hali halisi. Hujikuta wakitumia nguvu na maarifa mengi kutaka kuhakikisha yule ampendaye anakuwa wake. Stori hukolea zaidi likitokea na hili pia.

Yule anayempenda naye kutokuwa na mapenzi naye. Huwa linazuka balaa jipya. Ambalo wengi huwa hatujui namna ya kuhusika nalo na matokeo yake tunakuwa tunafurahia hali hii.

Wengi huwa tunaamini kwa kuwa kakataliwa na yule ampendaye kwa dhati basi ni nafasi ya dhahabu kurudi kwetu na kufurahia maisha. Huwa hivyo.

Huwa wanakuja kwetu kwa kuwa wanajua tunawapenda kwa kiwango kikubwa.

Ila hapa kuna kitu huwa tunakisahau na mara nyingi kinatugharimu.

Wengi wanapokuwa katika mahusiano ya namna hii. Ya kumkubali mtu baada ya kuiona alipopenda kashindwa kupendwa.

Huwa wanasumbuliwa na maumivu, huzuni na kujiona hawana thamani. Katika hali ya kawaida huwa wanahitaji faraja na kuoneshwa thamani ili kumbu kumbu za mwanzo ziweze kufutika katika vichwa vyao. Hapo sasa!

Baada ya kuwa katika mahusiano kwa muda mrefu na kusahau maumivu na karaha alizopata kutoka kwa yule aliyekuwa akimpenda. Huanza sasa na yeye kujihisi tofauti. Huanza kuona kama hustahili kuwa tena mpenzi wake.

Huanza kujiona kama yuko katika utumwa hivi, japo kiwango chako cha upendo kwake kinaweza kuwa hakijapungua zaidi ya kuongezeka pengine.

Taratibu visa na dharau kiasi huanza kushika hatamu.

Zile ‘dear’ na ‘sweetie’ zilizokuwapo mwanzo kwa wingi zinaanza kuota mbawa. Zile ‘sms’ na simu za kila mara nazo pia huanza kuyeyuka. Penzi limepea!

Katika hali hii wengi huwa tunajikuta tukianza lawama nakuona wahusika kama watu wasio kuwa na fadhila na utu. Tunaanza kuwaona kuwa ni watu wasiojua thamani ya kuthaminiwa na kujaliwa. Tunakuwa tumekosea kitu.

Mapenzi si kitu cha kulipana fadhila. Mapenzi si suala la kukumbuka ahadi na zawadi. Mapenzi ni hisia.

Mwanzo alipokuwa akikataa kuwa na wewe ni kwa sababu hakuwa na hisia na wewe. Ila hukukubali.

Uling’ang’ania na mwishowe ukatimiza kwa kuwa pamoja naye katika mazingira yasiyo kuwa ya kimapenzi hasa. Nasema hivi kwa sababu ulimchukua kipindi ambacho alihitaji kupozwa na kupewa faraja.

Katika kipindi hicho hata kama usingekuwapo angemkubali mwingine yeyote ambaye angeonekana kama anaweza kumfuta machozi na kumfanya afurahi. Ni kipindi alichohitaji faraja.

Katika kipindi hiki ubongo hufanya kazi zaidi ya kumtafuta mfariji huku hisia zikiwa zimeganda kwa maumivu ya kukataliwa. Mapenzi ni kupendana. Si suala la kuoneana huruma wala kuangalia historia. Hata kama unampenda kwa kiwango gani ila ikiwa hana hisia na wewe atajionea usumbufu tu.

Ndivyo mapenzi yalivyo. Hata kama ungekuwa wewe ungefanya hivyo. Huwezi kulazimisha hisia kumpenda mtu usiyempenda. Ni lazima mwisho uchemke tu.

Usikurupuke kuanzisha mahusianao na mtu wa aina hii.

Wengi wao hujikuta wakianzisha mahusiano kwa lengo la kupata faraja japo kwa wakati mwingine wao wanakuwa na hamu ya kutaka kupenda kweli. Ila hisia huwa zinakataa.

Wengi baada ya kupata faraja, amani na kuwasahau zilipendwa wao, nafsi zao nao hushtuka na kugundua hazipo kwa mtu ambaye si stahili halisi wa nafasi.

Huenda akathamini upendo wako na kila kizuri unachomfanyia lakini asiwe na hamu ya kuwa tena na wewe.

Kwa sababu anakuwa hana hisia na wewe. Kwa kuwa nafsi yake ikiwa na wewe inakuwa haipati faraja na raha inayopatikana baina ya wapendanao. Kwa leo hapa inatosha au sio?

  ramadhanimasenga@yahoo.com

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU