TUMESHINDWA KWENYE SOKA TUGEUKIE MICHEZO MINGINE.

TUMESHINDWA KWENYE SOKA TUGEUKIE MICHEZO MINGINE.

260
0
KUSHIRIKI

download (3)

NA SHARIFA MMASI

MWNARIADHA Alphonce Simbu, amefanikiwa kuleta medali ya shaba nchini, baada ya kushika nafasi ya tatu katika mbio za Marathon za riadha ya Dunia inayoendelea, London, England.

 

Medali ya shaba ambayo Simbu alishinda imeondoa ukame wa miaka 12 tangu Christopher Isegwe kushinda medali ya fedha katika mbio hizo hizo za marathon mashindano ya dunia yalipofanyika jijini Helsinki, Finland.

 

Historia sasa inaonyesha katika miaka 34 tangu mashindano ya riadha ya dunia yaanzishwe na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF), Tanzania inajivunia medali mbili tena katika mbio ndefu za marathon.

 

BINGWA tuna kila sababu ya kupongeza Simbu kwa kile alichokifanya Simbu Jumapili iliyopita  jijini London, kwani amekuwa ni mfano mkubwa kwa wanamichezo wengine.

 

Tunaona kwamba wanamichezo wengine wanatakiwa kujifunza kupitia mwanaridha huyo alianza kufanya vizuri kwenye mashindano mengine ya kimataifa.

 

Pamoja na juhudi zake binafsi za kufanya vizuri kwenye mashindano hao,  tunaona ushindi wake ni wa Watanzania wote na tuna kila sababu ya kuendelea kumpongeza.

 

Kwa sababu hivyo kila Mtanzania wanatakiwa ajione ni sehemu ya mafanikio ya Simbu kutokana na miaka mingi Tanzania imeshindwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

 

Tukiwa tunaanza kuona mafanikio kwenye michezo mingine kama riadha ni wakati sasa Watanzania kugeukia kusaidia kuliko kuendelea kudhamini soka pekee yake.

 

Tunasema hivyo  tukijua kwamba kwamba miaka mingi sasa katika soka hakuna mafanikio yoyote yaliyopatika pamoja na Watanzania  kujitokeza kusaidia mchezo huo.

 

Watanzania wakiwa watazamaji wa timu za wenzetu kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa na hiyo inatokana na timu yetu ya Taifa Stars kutolewa mapema katika hatua ya awali.

 

Kwa mara ya mwisho Tanzania ilishiriki fainali za Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 1980 zilizofanyika nchini Nigeria na tangu hapa haijawahi kufuzu tena, licha ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa wadau.

 

Kutokana na kupoteza mwelekeo kwenye soka  ni vema sasa tukageukia kusaidia michezo mingine kama riadha inayoleta sifa kwa Taifa kuliko kuendelea na soka.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU