BOSSOU AWATUMIA UJUMBE MZITO YONDANI, ‘CANNAVARO’

BOSSOU AWATUMIA UJUMBE MZITO YONDANI, ‘CANNAVARO’

2349
0
KUSHIRIKI

imagesBEKI wa zamani wa Yanga, Vincent Bossou, amewatumia ujumbe mzito mabeki wa timu hiyo, Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kuweka heshima katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba itakayochezwa Agosti 23, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana  kwa simu akiwa nchini Togo, Bossou, alisema mechi hiyo ni muhimu kwa kushinda ili kulinda heshima ya klabu hiyo kwa kutofungwa na Simba.

Bossou alisema amesikia uwepo wa mshambuliaji hatari Simba kama  Emmanuel Okwi, John Boko katika kikosi chao, hivyo kuwataka Yondani na Cannavaro kuhakikisha hawafurukuti kwenye mechi hiyo.

“Ni mechi muhimu natamani ningekuwapo niwaonyeshe kazi, lakini kwa bahati mbaya sipo tena huko waambie Yondani na ‘Cannavaro’ wajitoe wacheze kwa kujituma ili heshima irudi,” alisema Bossou.

Alisema Yondani na Cannavaro wamebeba jahazi katika suala zima la ulinzi wa timu hiyo.

“Nimesikia Simba wamesajili wachezaji wengi wazuri, isiwatishe hata kidogo wakiamua wanaweza kufanya kweli wapambane washinde,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU