BRAZIL WAMEPANDA VIPI NAFASI YA KWANZA VIWANGO VYA FIFA?

BRAZIL WAMEPANDA VIPI NAFASI YA KWANZA VIWANGO VYA FIFA?

697
0
KUSHIRIKI

brazil-football-story_650_060914083003ZURICH, Uswisi

SHIRIKISHO la Soka duniani (Fifa), wiki hii lilitoa orodha mpya ya viwango vya mataifa mbalimbali duniani lakini kumekuwa na ukakasi kuhusu namna gani Brazil ilivyoweza kutinga nafasi ya kwanza.

Brazil ilirudi kileleni mwa orodha hiyo baada ya kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwakani.

Hata hivyo, Brazil haijacheza mechi yoyote tangu Juni mwaka huu walipotandikwa na wapinzani wao Argentina katika mchezo wa kirafiki.

Lakini, kutokana na ushindi wao kwenye mechi mbili za kusaka tiketi ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay na Paraguay ambazo walicheza Machi 23 na 28 mwaka huu, ndizo zilizowawezesha kuishusha Ujerumani kileleni.

Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa kombe hilo, ilikuwa timu ya kwanza kujikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo ya mwakani itakayoandaliwa na Urusi.

Hata hivyo, imeshangaza kuona kwamba Brazil imerudi kileleni licha ya kumaliza nafasi ya nne kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2014 ambayo waliyaandaa wenyewe, kwani matokeo ya kila timu kwa zaidi ya miaka minne ndiyo yanayotumika kuchuja viwango  vya Fifa.

Mara ya mwisho kwa Brazil kunyakua taji la michuano hiyo ilikuwa mwaka 2002.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Ujerumani, ambao pia walinyakua Kombe la Mabara nchini Urusi wiki chache zilizopita wakitarajia kukutana na Brazil Machi mwakani, wameporomoka nafasi moja hadi ya pili huku Uswisi na Poland zikipanda nafasi ya nne na ya tano.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU