ESHA BUHETI ADAI WATOTO NI UTAJIRI

ESHA BUHETI ADAI WATOTO NI UTAJIRI

371
0
KUSHIRIKI

download (6)NA KYALAA SEHEYE

SIKU chache baada ya kujifungua mtoto wa kike, msanii wa filamu nchini, Esha Buhet, amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa zawadi hiyo kwani kupata mtoto wa jinsia yoyote ile ni utajiri mkubwa.

Esha ameliamba Papaso la Burudani kuwa familia yake imezidi kuongezeka kwani mwanawe wa kwanza anayeitwa Clarisa amepata mdogo wake hivyo kuwa na watoto wawili wa kike.

“Nashukuru Mungu mwanangu Clarisa amepata ndugu yake, hivyo familia imeongezeka inakuwa moja ya familia yenye utajiri na baraka kutoka kwa Mungu, kwani kuna watu wanatamani watoto lakini hawapati hivyo najivunia mno kupata warembo,” alisema Esha.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU