GYAN: NAWAJUA YANGA

GYAN: NAWAJUA YANGA

2607
0
KUSHIRIKI

Asamoah_Gyan_(2014)NA CLARA ALPHONCE

WAKATI homa ya mchezo wa Simba na Yanga ikiwa imeanza kupanda kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo, mshambuliaji mpya wa timu ya Simba, Nicolaus Gyan kutoka Ghana, ameibuka na kudai kuwa anawajua vizuri wapinzani wao Yanga.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Agosti 23 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Gyan ambaye kwa sasa ameondoka nchini na kurejea kwao baada ya kumalizana na Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili, anatarajia kurejea tena nchini Agosti 30, au Septemba 2 baada ya kumaliza mkataba wake na timu yake.

Alisema Yanga ni timu nzuri lakini si ya kuwatisha kutokana na kikosi cha Simba alichokiona kwenye tamasha lao lililofanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

“Yanga nawajua, niliwaona kwenye mchezo wao na Medeama ya Ghana kwenye Ligi ya Mabingwa, si timu mpya kwangu najua wanavyocheza, hivyo na imani naweza kuwafunga siku hiyo kama nitapata nafasi ya kucheza,” alisema Gyan.

Alisema kwa mara ya kwanza anacheza soka nje ya Ghana, ila amefurahishwa na mashabiki wa Simba kwa kumpokea vizuri na yeye anawaahidi mazuri.

“Ghana kuna ushabiki ila hapa nimeona ni zaidi, nimefurahi Simba wamenipokea vizuri, nami nitajitahidi kila nikipata nafasi ya kucheza nifunge ili kulipa fadhila zangu kwao,” alisema Gyan.

Pia mchezaji huyo aliwashukuru Idd Kajuna ambaye ni Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, wakala Juma Ndabile, kwa kuona uwezo wake na kumleta Simba.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU