JULIO AMVUTA BEKI WA SIMBA POLISI FC

JULIO AMVUTA BEKI WA SIMBA POLISI FC

747
0
KUSHIRIKI

 

download (5)NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

KOCHA wa Polisi Dodoma, Jamhuri Kihwelo, amemsajili beki wa zamani wa Simba, Masoud Nassoro ‘Chollo’, katika kikosi chake kitakachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Julio alitambulishwa rasmi jana mjini hapa  na Katibu Mkuu wa Polisi FC, Fortunatus John, kuwa ni kocha mpya wa kikosi chao.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Julio alisema atahakikisha anaipandisha timu hiyo daraja ili iweze kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu wa 2018/19.

Alisema malengo yatatimia kama atapata ushirikiano kutoka kwa wananchi na uongozi wa mkoa huo.

“Mimi huwa sipendi kushindwa napenda timu ya ushindi, naomba ushirikiano kutoka kwa wananchi, kwani nimesikia timu hii ni ya wananchi,” alisema Julio.

Julio alisema katika kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri, amefanya usajili wa beki mzoefu za zamani wa Simba, Cholo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Alisema ameamua kumsajili Cholo kutokana na uzoefu alionao katika ligi mbalimbali alizocheza akiwa na timu tofauti nchini.

“Ili upandishe timu lazima uwe na wachezaji wenye uzoefu pamoja na damu change, sasa mimi nimeweka mchanganyiko nikiamini watanisaidia katika ligi hiyo,” alisema.

Aliwataja wachezaji wengine wenye uzoefu waliosajiliwa katika timu hiyo ni Jackson Chove, John Mbise, Lusajo Mwakasagule, Seleman Kibuta na Abdallah Chambala.

Wengine ni Anorld Raurent, Jamal Machelenga, Malick Kapolo, James Mendi, Rajabu Habibu, Ibrahim Ngecha, Benjamin Charles, Hussein Abdallah na Benedictor William.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU