KATAUTI: MASHABIKI HAWATAMPA PRESHA NIYONZIMA

KATAUTI: MASHABIKI HAWATAMPA PRESHA NIYONZIMA

1189
0
KUSHIRIKI

ftzuOnllNA WINFRIDA MTOI

MCHEZAJI wa zamani wa Yanga  ambaye ni Kocha Msaidizi wa Ryon Sport ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, amesema  Haruna Niyonzima hawezi  kuyumbishwa na presha za mashabiki pindi zitakapokutana timu za Simba na Yanga, Agosti 23.

Niyonzima aliyesajiliwa na Simba  msimu huu akitokea Yanga, alicheza mechi yake ya kwanza  akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi katika Tamasha la Simba Day lililofanyika Agosti 8, mwaka huu  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA, Ndikumana alisema mchezaji huyo amepitia mambo mengi hivyo si rahisi kuogopa wingi wa mashabiki watakaofika uwanjani hapo na kumfanya acheze chini ya kiwango.

“Hata kama watu hawajafurahishwa na yeye kuondoka kwenda Simba,  Haruna ni mchezaji mkubwa na usitegemee kama atafanya vibaya kutokana na presha ya mashabiki, atacheza kama  alivyozoea,” alisema.

Alisema hata Rwanda anakotoka mashabiki wake wengi hawakufurahishwa na yeye kwenda Simba, lakini mpira ni kazi mchezaji yupo huru kucheza timu yoyote anapoona atapata nafasi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU