KUMBE KIDUMU WA RIHANNA AMEOA BWANA

KUMBE KIDUMU WA RIHANNA AMEOA BWANA

266
0
KUSHIRIKI

images (2)LONDON, England

RIHANNA ameonekana kujitahidi sana kutunza siri juu ya uhusiano wake na bilionea la Saudi Arabia, Hassan Jameel kwa muda wa takribani miezi sita.

Lakini, hali halisi ni kwamba, Jameel anayeonekana kupenda sana ‘totooz’, naye ni mzuri wa kutunza siri hasa zile nzito nzito ambazo Rihanna mwenyewe asingeweza kuzijua.

Mtandao wa The Sun uliripoti kuwa, bilionea huyo, Hassan, ambaye familia yake inamiliki haki za biashara za magari ya Toyota, alikuwa na ndoa kabla hata hajaanza mahusianoa ya kimapenzi na Rihanna.

Ni wazi kuwa, huenda bilionea huyo akaanzisha hata mahusiano mengine na Rihhana asijue, kama alivyofanya kwa mkewe Lina Lazaar, mtaalamu wa sanaa ambaye alifunga naye pingu za maisha mwaka 2012 na kufanya sherehe kubwa kwenye jumba la Paris Opera, Paris, Ufaransa.

Chanzo kimoja cha habari kiliutonya mtandao wa The Sun: “Hassan ni kiumbe mmoja anayependa sana kutunza siri.

“Ndoa yake ilishavunjika kabla hata hajakutana na Rihanna, Lina ndiye aliyemuacha, ni habari za kushtusha lakini.

“Hata hivyo, Lina naye ana mpenzi mwingine kwa sasa.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU