‘MECHI ZA SIMBA, YANGA HUCHEZWA NJE YA UWANJA’

‘MECHI ZA SIMBA, YANGA HUCHEZWA NJE YA UWANJA’

850
0
KUSHIRIKI

yanga-vs-simba-01102016_xanfqo3qb9ii1io2ucsv57mkpNA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa zamani wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, amesema siku zote mechi za watani wa jadi Simba na Yanga huwa zinachezwa nje ya uwanja.

Mmachinga ameyasema hayo zikiwa zimesalia siku 11 kuchezwa kwa mechi ya watani hao, ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu unaokuja.

Akizungumza na BINGWA jana, Mmachinga alisema mara nyingi mechi za Simba na Yanga hubeba mambo mengi yanayoonekana kwa macho na yasiyoonekana.

Alisema kabla ya mchezo unaweza kusikia tambo kutoka pande hizo mbili, kufanyika vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina hivyo vyote ni katika kuitoa mchezoni timu moja.

“Siku zote katika mechi hizo mwenye kumzidi mwenzake ujanja ndiye mshindi,  ndio maana inakuwa ngumu na hata kufikia hatua mara baada ya mchezo upande mmoja ulioshindwa huvurugana kwa kulaumiana.

“Ukifuatilia vizuri mechi baina ya timu hizo na kama una imani ya Mungu unaweza kuuchukia mpira, lakini mwisho wa siku yote yanayofanywa ni kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wao,” alisema.

Simba na Yanga zitakuwa dimbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Agosti 23, mwaka huu, kufungua pazia la ligi msimu wa 2017/18.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU