MNA SWALI KWA REAL MADRID?

MNA SWALI KWA REAL MADRID?

306
0
KUSHIRIKI

Real.Madrid.vs.Man.United.533x300.690x400MADRID, Hispania

KWA kuitandika Manchester United kwenye fainali ya UEFA Super Cup mjini Skopje, Macedonia, klabu ya Real Madrid kwa sasa hautakosea kuwaita wababe wa soka la Ulaya.

Hapo awali, wakongwe wa Madrid ambao waliifanikisha timu hiyo kunyakua mataji matano mfululizo ya Ulaya kati ya mwaka 1956 na 1960, walitamba kuwa rekodi yao haitavunjwa, lakini Real Madrid ya sasa inaonesha balaa na kwa kutwaa mataji matatu ya Ulaya ndani ya miaka minne ya mwisho.

Tangu Shirikisho la Soka barani humo (UEFA) lianzishe michuano ya ngazi ya klabu, kumekuwa na fainali 189 za michuano yote waliyoiandaa, ambapo Real Madrid iliibuka na ushindi kwenye fainali 18: 12 za Ligi ya Mabingwa, mbili za UEFA Cup na nne za UEFA Super Cup.

Kwa jinsi ambavyo rekodi zao zinatisha Ulaya, hata lile kombe limeanza kufanana nao.

Hadi sasa, Los Blancos hao wamefanikiwa kutwaa mataji sawa na idadi ya timu za England na Italia, mataji matano zaidi ya timu za Ujerumani na sita zaidi ya zile za Uholanzi.

Kwa hali hiyo basi, hatutokosea kusema Real Madrid huwa haichezi fainali za Ulaya, bali huwa inashinda fainali za Ulaya. Ni haki yao kupewa hata taji kabla hawajacheza.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU