SIKIA KISA CHA IRAN KUWAFUNGIA WACHEZAJI WAKE

SIKIA KISA CHA IRAN KUWAFUNGIA WACHEZAJI WAKE

281
0
KUSHIRIKI

hi-res-0248c45f2991cc671f9c94c264db20cd_crop_northTEHRAN, Iran

TIMU ya taifa ya soka ya Iran imewapiga marufuku wachezaji wake wawili kuitumikia timu hiyo baada ya kudaiwa kucheza mechi dhidi ya klabu ya Israeli kwenye Ligi ya Europa.

Taarifa hiyo ilithibitishwa na msemaji wa serikali ya Iran, ambapo nyota waliopewa adhabu hiyo ni nahodha Masoud Shojaei mwenye umri wa miaka 33 na kiungo Ehsan Haji Safi, 27.

Nyota hao wanaoichezea klabu ya Panionios ya Ugiriki dhidi ya Maccabi Tel Aviv ya Israel wiki iliyopita.

Iran haiitambui Israel kama taifa na imewazuia wanamichezo wao kucheza dhidi ya timu zote za Israeli.

“Ni kweli kabisa, Masoud Shojaei na Ehsan Haji Safi hawatoshirikishwa kuichezea timu ya taifa kutokana na kuvuka mipaka,” alisema Naibu Waziri wa Michezo wa Iran, Mohammad Reza Davarzani.

“Sawa ni wachezaji wa kulipwa huko, lakini kucheza dhidi ya timu ya Israeli ni jambo lisilokubalika kwa watu wa Iran.”

Shojaei, ambaye ameiwakilisha Iran katika mechi 70 za kimataifa, alikuwa mmoja wa wachezaji walioisaidia timu hiyo kufuzu Kombe la Dunia mwakani.

Haji Safi, ambaye ameichezea Iran mechi 84, alikuwa kwenye benchi Juni wakati timu yake ikivaana na Uzbekistan na kupata ushindi, huku akitegemewa kuiwakilisha timu yake hiyo mwakani nchini Urusi.

Aidha, Shojaei alishawahi kuikera serikali ya Iran Juni mwaka huu kwa kumuomba rais wake, Hassan Rouhani kuwaruhusu wanawake waingie viwanjani kutazama soka, jambo ambalo lilikatazwa nchini humo tangu mwaka 1979.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU