TAMMY AMWAGA SIRI ZA JAY MOE

TAMMY AMWAGA SIRI ZA JAY MOE

404
0
KUSHIRIKI

tammy-2NA CHRISTOPHER MSEKENA

RAPA machachari wa kike nchini, Tamari Ally ‘Tammy The Baddest’, amesema siri ya kumshirikisha Jay Moe kwenye wimbo wake mpya unaoitwa Chapaa, ni kutokana na jinsi anavyomwelewa zaidi mwana hip hop huko mkongwe.

Tammy ameliambia Papaso la Burudani kuwa amekuwa akimsikiliza Jay Moe kwa muda mrefu hivyo alivyopata nafasi ya kuwa naye karibu hakusita kumwomba atupie mistari kadhaa kwenye wimbo wake huo.

“Huwa namwelewa sana Jay Moe kwenye kazi zake, nilipokutana naye studio nilimuuliza kiutani kwanini tusifanye ngoma, akakubali basi tukarekodi Chapaa ambayo nimeitoa wiki hii na ninashukuru imepokewa vizuri na mashabiki,” alisema Tammy.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU