WOLPER AFURAHIA MATUNDA YA KUJIFUNZA KUSHONA

WOLPER AFURAHIA MATUNDA YA KUJIFUNZA KUSHONA

406
0
KUSHIRIKI

download (4)Na BRIGHITER MASAKI

BAADA ya kufungua duka la nguo lijulikanalo kama Wolper Stylish, msanii nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper, amewapa pole wale wote waliokuwa wanamcheka kipindi anajifunza kushona na cherehani.

Mrembo huyo ameliambia Papaso la Burudani kuwa anajihisi mwenye bahati na hakukosea kwenda kujifunza kushona kwa cherehani ambapo sasa hivi anaziuza nguo anazozishona kwa khanga na vitenge katika duka lake.

“Nawapa pole sana wale wote waliokuwa wakinicheka kipindi najifunza kushona kwa cherehani, wengine wakaniambia nimefulia sina jipya, lakini kwa sasa wanaona mafanikio ninayopata, nimetoa ajira kwa vijana na popote ukiona nimevaa nguo ya kitenge au khanga basi ujue nimeshona kwa mkono wangu, nawashonea na wengine pia kwa bei nafuu, watu waje Wolper Stylish wapendeze,” alisema Wolper.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU