Ali Kiba, P Square, Cassper Nyovest jukwaa moja

Ali Kiba, P Square, Cassper Nyovest jukwaa moja

523
0
KUSHIRIKI
Ali Kiba
Ali Kiba
Ali Kiba

NA CHRISTOPHER MSEKENA
MSANII staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba, kesho anatarajia kuungana na mastaa wa muziki barani Afrika katika tamasha la watu weusi wanaoishi Marekani, lijulikanalo kama One Africa Music Festival 2017, litakalofanyika kwenye Uwanja wa Amphitheatre Coney, Brooklyn, New York nchini humo.
Ali Kiba, ambaye hivi karibuni anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Kipusa, atatumbuiza kwenye jukwaa moja na wasanii wakali Afrika kama vile kundi la P Square, Cassper Nyovest, 2 Face pamoja na Tiwa Savage.
Mastaa wengine wa muziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo la One Africa linalofanyika kila mwaka ni Tekno, Mr Flavour, Victoria Kimani, Davido, Banky W na Timaya.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU