TETESI ULAYA: IBRAHIMOVIC AJIPA MKATABA MAN U

TETESI ULAYA: IBRAHIMOVIC AJIPA MKATABA MAN U

558
0
KUSHIRIKI

Gerrard awaonyesha Liver beki wa kati

MERSEYSIDE, England

KIUNGO wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard, amewataka mabosi wa timu hiyo kumsajili Virgil Van Dijk.

Kwa mujibu wa mkongwe huyo, Liver wanamhitaji kwa namna yoyote beki huyo wa kati wa Southampton.

Ibrahimovic ajipa mkataba Man U

MANCHESTER, England

STRAIKA Zlatan Ibrahimovic amesema yuko tayari kusaini mkataba mpya mapema wiki hii.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni miezi michache tangu alipotemwa kikosini baada ya kuumia goti.

Jina la Draxler latua Anfield

MERSEYSIDE, England

MABOSI wa Liverpool wameanza kumzungumzia staa wa PSG, Julian Draxler ambaye anataka kuondoka Ufaransa.

Mjerumani huyo alicheza mechi 17 pekee msimu uliopita na haonekani kuwa na nafasi msimu huu.

‘Barca mnajisumbua bure kwa Dembele’

MUNICH, Ujerumani

MTENDAJI Mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke, amewaambia Barcelona wasijisumbue kumfukuzia staa wake, Ousmane Dembele.

Nyota huyo amekuwa akitakiwa Catalunya lakini Dortmund wameshaitolea nje ofa yao ya pauni milioni 90.

Nasri asajiliwa na Waturuki

MANCHESTER, England

NYOTA wa Manchester City, Samir Nasri, amewasili nchini Uturuki kumalizana na mabosi wake wapya wa Antalyaspor.

Nasir ameshindwa kupenya kwenye mipango ya Pep Guardiola, hata baada ya msimu uliopita kucheza Sevilla kwa mkopo.

Wenger atangaza kupiga bei mastaa

LONDON, England

KOCHA Arsene Wenger amesema atauza baadhi ya wachezaji wake kabla ya kufungwa kwa dirisha hili la usajili.

Mpaka sasa, Gunners wamechukua wachezaji wapya wawili tu ambao ni Alexander Lacazette na Sead Kolasinac.

Nyota Lazio akataa kwenda England

TURIN, Italia

NYOTA wa Lazio na timu ya Taifa ya Senegal, Keita Balde, hana mpango wa kutua Ligi Kuu England na badala yake atajiunga na Juventus.

Balde anatakiwa na West Ham lakini Juve wanapewa nafasi kubwa ya kumchukua.

Conte kung’oa mtu Tottenham

LONDON, England

IMERIPOTIWA kuwa Chelsea wanaangalia uwezeakano wa kumsajili beki wa Tottenham, Toby Alderweireld.

Alderweireld amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha Spurs tangu alipotua mwaka 2015 akitokea Atletico Madrid.

Leicester wamsubiri winga wa Palace

LONDON, England

LEICESTER City wako kwenye hatua za mwisho katika kukamilisha usajili wa winga wa Crystal Palace, Andros Townsend.

Palace wameshaanza harakati za kuiwania saini ya Oliver Burke wa RB Leipzig kuziba pengo la Townsend.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU