DUNIA YA MKE WANGU

DUNIA YA MKE WANGU

374
0
KUSHIRIKI

Ilipoishia

“Sikutanii mke wangu, kwani nimefanikiwa kupata dawa ya Ebola,” aliongea Kai na kumuweka mke wake mdomo wazi akimshangaa asiamini ayasemayo.

 “Je, kwa sasa unahisi tofauti yoyote katika mwili?” Kai aliuliza.

 Julia alijitazama mwili wake na kujibu.

 “Ni kweli mwili wangu ni mwepesi tofauti na mwanzo.”

SASA ENDELEA

“UMEPONA mke wangu. Baada ya siku tatu utakuwa mzima kabisa.”

Upesi Julia alimkumbatia Kai na kumshika kwa nguvu. Alilia sana asiamini kama mume wake amefanikiwa  katika hilo. Furaha isiyoelezeka kwa urahisi iliingia ndani ya nyumba hiyo. Hali ya tofauti aliyokuwa akiihisi Julia ilimfanya aamini ayasemayo Kai.

“Mume wangu unaamini kweli kuwa dawa uliyoigundua itaniponya kabisa,” aliuliza Julia.

“Mke wangu amini itakuponya nimeshaithibitisha vya kutosha kuwa dawa hii inaua virusi vya primase,” alijibu Kai akiwa amemshika Julia mashavuni.

“Hakika wewe ni mwanaume usiyeshindwa. Asante kwa kunirudisha duniani. Nakupenda sana mume wangu,” aliongea Julia akilia sana.

“Unajua kabisa kuwa siwezi kuishi bila wewe. Sielewi kama ningekuua endapo ningekuwa nimeikosa dawa hii, sijui kama ningejaribu kufanya hivyo. Nakupenda sana mke wangu. Namshukuru Mungu kwa kuweza kukurudisha tena katika dunia hii,” aliongea Kai akitokwa na machozi ya furaha.

Walikumbatiana kwa muda mrefu na mashozi ya furaha yakitiririka machoni mwao. Furaha ya wanandoa wanaopendana kati ya mwanasayansi Kai Luda na Dk. Julia Fenarndo, ilirudi upya na kwa kishindo kikubwa. Julia alishindwa kumtafakari mume wake kwa jinsi alivyopamabana.

Kai aliendelea kumhudumia mkewe, akimpigia vyakula vizuri na kumpa dozi ya dawa, dawa ya Sanbira tricony. Uzuri halisi wa Julia ulianza kurejea, damu zilizokuwa zikimtoka sehemu zote zenye matundu, zilianza kupungua. Alimchukua vipimo maalumu ili kujua uajuzito wake ulikuwa ukiendelea vipi. Watoto walionekana wakicheza tumboni. Furaha ya Kai iliongezeka maradufu, alifanya maombi maalumu yeye na Julia, wakimshukuru Mungu kwa muujiza wake.

Siku ya pili Kai alimpelekea Julia ufukwe wa bahari. Alimbeba mgongoni mwake, akimfanyisha mazoezi. Walicheza na kufurahi, bado ilikuwa ngumu kuamini kama ni kweli maisha yao yalikuwa yamerejea.

Baada ya siku nne, Julia alipona kabisa. Kwa mara ya kwanza tokea Kai arudi kutoka Ethiopia, alikokwenda kumtafuta Julia, aliwapigia simu wazazi wake na kuwajulisha  kuwa yeye na Julia walikuwa nyumbani. Wazazi wa Kai hawakuamini upesi walifunga safari hadi nyumbani kwao kwenda kuwaona watoto wao.

Mama yake na Julia alimkimbilia mwanaye na kumkumbatia. Julia alimsimulia mama yake kila kitu kilichomkuta akiwa nchini Ethiopia.

“Nisamehe mama mimi ni mkosaji sikukwambia kuwa nakwenda Keneza,” aliongea Julia akilia kwenye kifua cha mama yake.

“Usilie mwanangu. Nimesikia ulichowafanyia watoto wa kijiji cha Keneza, hongera sana,” alijibu mama yake.

Mzee Luda alimkumbatia mwanaye. Kai alikaa na baba yake na kumueleza kuwa  Julia amemfanya agundue dawa ya Ebola.  Mzee Luda alichukua muda kuamini kama kweli mwanaye alikuwa amefanikiwa kugundua dawa ya Ebola.

Sherehe kubwa ilifanyika nyumbani kwa Kai. Serikali ilijulishwa kuwa mwanasayansi Kai Luda alikuwa amerejea kutoka Ethiopia pamoja na mkewe. Rais aliwaita Kai na Julia Ikulu. Vyombo vya habari vilianza kutangaza habari zilizomhusu Kai na mkewe Dk. Julia. Shirika la Utangazaji la BBC lilikuwa la kwanza kurusha matangazo likiujilisha ulimwengu kuwa Kai alikuwa amefanikiwa kumtoa mkewe nchini Ethiopia.

Kai aliingia kwenye tovuti ya wanasayansi na kuwajulisha kuwa alikuwa amefanikiwa kugundua dawa ya Ebola, pamoja na kinga ya ugonjwa huo. Wanasayansi kote duniani, walipozipata taarifa hizo, hawakuamini mara moja. Mkuu wa Idara ya Sayansi, Dk. Mark Vin, alitoa taarifa hiyo kwa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kai aliandika viunganishi alivyovitumia wakati wa utengenezaji wa dawa ya Sanbira tricony, pamoja na kinga yake. Alituma ujumbe mfupi kwa Dk. Mark Vin. Dk. Mark aliutuma ujumbe huo kwa kiongozi wa maabara kuu ya dunia. Maabara kuu ya dunia ilianza majaribio ya kuthibitisha kama viunganishi hivyo vilikuwa vinaleta kweli dawa ya kutibu ugonjwa hatari wa Ebola.

Siku ya nne wanasayansi kutoka maabara kuu ya dunia waliuthibitishia ulimwengu kuwa dawa ya Ebola ilikuwa imepatikana. Picha ya mgunduzi wa dawa ya Ebola iliwekwa wazi. Kai alionekana kwenye vyombo vyote vya habari. Majarida mbalimbali yalimwandika Kai kama shujaa wa Afrika.

Upesi dawa hiyo ilianza kutengenezwa kwa wingi na kusambazwa kote duniani. Nchi ya Ethiopia ilikuwa ya kwanza kupatiwa dawa ya Sanbira tricony. Mamilioni ya watu walianza dozi ya dawa hiyo. Wengi walipona na kurudi kwenye maisha yao ya kawaida. Hata wale wagonjwa ambao baadhi ya viuongo vyao vilikuwa vimeoza na kukatika, walipona, japo miili yao ilibaki kuwa na makovu.

Dawa hiyo ilikuwa ni dawa yenye nguvu na ya ajabu, kwani ilikuwa na uwezo wa kumponya mtu kwa muda mfupi.

Baada ya miezi mitatu, Julia alijifungua mtoto wa kiume na wa kike. Mapacha hao waliongeza furaha zaidi kwenye ukoo wa mzee Luda. Mtoto wa kiume walimpa jina la Rogers na wa kike walimuita Rona.

Baada ya miezi miwili Kai alirudi chuoni London. Aliondoka na Julia pamoja na watoto wao.

Mwisho

Asante kwa kuwa pamoja na mimi katika simulizi hii ya kusisimua. Usikose hadithi nyingine kali zaidi, katika gazeti hili.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU