TETESI ULAYA: MAN CITY WAMTENGEA DAU NONO ‘FUNDI’ MESSI

TETESI ULAYA: MAN CITY WAMTENGEA DAU NONO ‘FUNDI’ MESSI

716
0
KUSHIRIKI

Man City wamtengea dau nono ‘fundi’ Messi

MANCHESTER, England

MANCHESTER City wamepania kumchukua Lionel Messi wakiwa wameandaa euro milioni 300 kumsajili.

Chanzo kimoja cha habari kimenyetisha kwamba, Messi alikutana na Pep Guardiola, mwaka jana kuzungumzia mpango huo.

Aubameyang ajipeleka mikononi mwa Zidane

MUNICH, Ujerumani

IMERIPOTIWA kuwa straika Pierre-Emerick Aubameyang, ameendelea kumpigia simu kocha Zinedine Zidane, akiulizia mpango wa kutua Real Madrid.

Inasemekana kwamba licha ya Aubameyang kuitaka Madrid, Zidane si shabiki wa mchezaji huyo.

Marseille nao wamtaka Dembele

MARSEILLE, Ufaransa

RAIS wa klabu ya Marseille, Jacques-Henri Eyraud, amefichua kuwa wanatolewa udenda na saini ya straika wa Celtic, Moussa Dembele.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 21, amewahi kuwa kwenye rada za wababe wa La Liga, Barcelona.

Blues wakaribia kunasa wawili 

LONDON, England

VIFAA viwili kutoka Leicester City na Inter Milan, vinakaribia kujiunga na wababe wa London, Chelsea.

Kiungo Danny Drinkwater wa Leicester atatua kwa pauni milioni 30 na Antonio Candreva wa Inter atagharimu pauni milioni 25.

Chamberlain, Arsenal bado hakijaeleweka

LONDON, England

BADO Arsenal hawana uhakika wa kumbakiza kiungo wao, Alex Oxlade-Chamberlain, kwani ameendelea kuugomea mkataba mpya.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akizitoa udenda klabu za Chelsea na Liverpool.

Liverpool wapanga kuibomoa Madrid

MERSEYSIDE, England

LIVERPOOL wamemgeukia kiungo wa Real Madrid, Mateo Kovacic na nia yao ni kumsajili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Mpango huo ni baada ya wakali hao wa Anfield kushindwa kuinasa huduma ya nyota wa Bundesliga, Naby Keita.

Mourinho kumrudia Griezmann mwakani

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, amepania kuufufua mpango wa kumchukua Antoine Griezmann, katika dirisha la usajili la mwakani.

Man United walishindwa kumsajili Griezmann kwakuwa Atletico Madrid walifungiwa kusajili, hivyo wakaamua kumbakiza nyota huyo.

Mangala alazimisha ‘shavu’ Inter Milan

MILAN, Italia

BEKI wa Manchester City, Eliaquim Mangala, ametajwa kutaka kuwaomba mabosi wake wamruhusu kwenda Inter Milan.

Beki huyo wa kati wa Inter mwenye umri wa miaka 26, alitarajiwa kukutana na uongozi wa Etihad jana.

Matuidi meno nje kusajiliwa Juventus

TURIN, Italia

KIUNGO mwenye umri wa miaka 30 aliyetua Juventus, Blaise Matuidi, ameonyesha kukunwa na usajili wake huo.

Matuidi aliyekuwa PSG, alijiunga na Juve siku chache zilizopita kwa ada ya usajili ya pauni milioni 18.5.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU