DONDOO ZA ULAYA; GUARDIOLA AMPIGIA HESABU AUBAMEYANG

DONDOO ZA ULAYA; GUARDIOLA AMPIGIA HESABU AUBAMEYANG

792
0
KUSHIRIKI

Nyota mpya awasili Barca

CATALUNYA, Hispania

MCHEZAJI mpya wa Barcelona, Ousmane Dembele, amefika klabuni hapo akitokea Ujerumani, kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Nyota huyo ametokea Borussia Dortmund iliyomruhusu kwa dau lililovunja rekodi yao ya mauzo ya pauni milioni 97.

Jovetic kumrithi Mbappe Monaco

MONACO, Ufaransa

HUKU kukiwa na dalili zote za kinda wao, Kylian Mbappe kwenda PSG, mabosi wa Monaco wanamfuatilia staa wa Inter Milan, Stevan Jovetic.

Jovetic mwenye umri wa miaka 27, aliwahi kuichezea Man City kabla ya kupelekwa Sevilla kwa mkopo na kisha kutua Inter.

Inter wamsubiri beki Arsenal

MILAN, Italia

INTER Milan wanaamini watafanikiwa kumsajili beki wa kati wa Arsenal, Shkodran Mustafi.

Beki huyo aliachwa kwenye kikosi cha Gunnres kilichobamizwa mabao 4-0 na Liver juzi.

Kipa Liverpool atakiwa Serie A

MERSEYSIDE, England

TAARIFA zimedai kwamba, saini ya mlinda mlango wa Liverpool inagombewa na vigogo wa Serie A, Napoli.

Uvumi huo umeongezeka zaidi baada ya kipa huyo kutocheza katika mchezo wa juzi dhidi ya Arsenal.

Remy agombewa Hispania, Italia

LONDON, England

FOWADI wa Chelsea, Loic Remy, anawaniwa na Las Palmas ya La Liga na wakati huo huo Cagliari ya Italia inamtaka.

Kwa upande wa klabu yake, imeanza kuangalia uwezekano wa kumchukua straika wa Swansea, Fernando Llorente.

Mkongwe amng’oa Mata Man United

MANCHESTER, England

MCHEZAJI wa zamani wa Chelsea, Pat Nevin, amemtaka Juan Mata kuondoka Manchester United kwani akibaki atakiua kiwango chake.

Mkongwe huyo anaamini Mata hawezi kung’ara kama ataendelea kuwa chini ya Jose Mourinho.

Guardiola ampigia hesabu Aubameyang

MANCHESTER, England

KOCHA Pep Guardiola, anavutiwa na huduma ya straika anayetaka kuondoka Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.

Imeelezwa kwamba, tayari Guardiola ameshazungumza na mabosi wake akiwaambia anamtaka Mwafrika huyo kwenye kikosi chake.

 Juventus wapewa beki Bundesliga

TURIN, Italia

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Matteo, ameiomba Juventus kumsajili beki wa Schalke 04, Benedikt Howedes.

Howedes alikuwa nahodha wakati Di Matteo alipokuwa akiinoa Schalke na ni mzuri anapocheza nafasi ya beki wa kulia na mlinzi wa kati.

Dortmund wapania  kumbeba Draxler

PARIS, Ufaransa

WAWAKILISHI wa Borussia Dortmund wako Ufaransa kuangalia uwezekano wa kusepa na kiungo, Julian Draxler wa PSG.

Hata hivyo, haitakuwa rahisi kwani Dortmund ni mahasimu wa klabu yake ya zamani ya Schalke 04.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU