MKONGWE ALDO AMFUATA MCGREGOR KISA MAYWEATHER

MKONGWE ALDO AMFUATA MCGREGOR KISA MAYWEATHER

353
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

BINGWA wa zamani wa ‘kick boxing’, Jose Aldo, amepanga kuhamishia makali yake katika ulingo wa ‘boxing’ kama alivyofanya Conor McGregor.

McGregor, ambaye ni staa wa ngumi na mateke, hivi karibuni alipigana pambano lake la kwanza la boxing dhidi ya Floyd Mayweather, licha ya kupoteza katika raundi ya 10.

Pambano hilo limemvutia Aldo, ambaye anaamini hata yeye anaweza kupanda ulingoni kuzichapa na mabondia wakubwa.

Aldo ameonekana akijifua zaidi ili kujiweka sawa kwa ajili ya mapambano ambayo inasemekana yameanza kuandaliwa.

Nyota huyo yupo mjini California katika ‘gym’ ya Roberto Garcia, ambaye pia ni staa wa zamani wa boxing.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU