ZIZZOU CHANZO MADRID KUMKOSA MBAPPE

ZIZZOU CHANZO MADRID KUMKOSA MBAPPE

540
0
KUSHIRIKI

MADRID, Hispania

HUENDA nyota Kylian Mbappe angekuwa mchezaji wa Real Madrid kwa sasa kama si Zinedine Zidane kutolewa kwenye majukumu ya kukinoa kikosi cha vijana klabuni hapo.

Zizou alihamishwa kutoka kwenye benchi la ufundi la makinda wa Castila na kupewa majukumu ya kuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti, jambo ambalo lilisababisha Mbappe kusita kwenda Madrid.

“Kama Zidane angebaki na kuwatazama makinda kama Kylian, tungekuwa tumehamia Madrid na si Monaco.”

Mbappe alikaribia kujiunga na Madrid akiwa na umri wa miaka 14 na aliwahi kufika Bernabeu na mwaka 2012  kukutana na Cristiano Ronaldo na Zidane, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kocha wa ‘academy’.

“Tulikutana mara nyingi na Zidane lakini ghafla alichaguliwa kuwa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza kuelekea msimu wa 2013-14.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU