TETESI ULAYA; GUARDIOLA AMTEGEA SANCHEZ MWAKANI

TETESI ULAYA; GUARDIOLA AMTEGEA SANCHEZ MWAKANI

451
0
KUSHIRIKI

Guardiola amtegea Sanchez mwakani

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amemkosa Alexis Sanchez, lakini amepanga kumrudia pindi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwakani.

Taarifa zilizopo ni kwamba, Man City watajaribu kumsajili Sanchez kwa mkopo Januari.

Bado kidogo Everton wangembeba Vermaelen

MERSYSIDE, England

EVERTON walitaka kumchukua beki wa Barcelona, Thomas Vermaelen, lakini wababe hao wa La Liga waligoma.

Imeripotiwa kwamba, Everton walimtaka nyota huyo wa zamani wa Arsenal kwa mkopo.

Mke ambakiza Giroud Arsenal

LONDON, England

MASHABIKI wa Arsenal wanapaswa kumshukuru mke wa straika, Olivier Giroud, kwani ndiye aliyezuia mchezaji huyo kuondoka.

Giroud mwenye umri wa miaka 30, alikaribia kutua Everton lakini mpango huo ulikwama katika dakika za mwisho.

Klopp alimtaka Chamberlain miaka mitatu iliyopita

MERSEYSIDE, England

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amekenua kumsajili kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, akisisitiza alimfuatilia kwa miaka mitatu.

Klopp ametoboa kwamba alianza kumtazama nyota huyo tangu alipokuwa akiinoa Borussia Dortmund.

De Boer ahofia kufukuzwa kazi

LONDON, England

KOCHA wa Crystal Palace, Frank de Boer, anahofia kukipoteza kibarua hicho licha ya kukipata wiki chache zilizopita.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, ameanza vibaya kibarua chake akiwa amepoteza mechi zake tatu mfululizo.

Lemar akenua kubaki Monaco

MONACO, Ufaransa

WINGA Thomas Lemar, ameeleza kufurahishwa kwake na kitendo cha kubaki Moanco licha ya kufukuziwa na vigogo.

Liverpool na Arsenal zilikuwa zikimfukuzia nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini hakuna iliyomnasa.

Sakho sasa rasmi Palace

LONDON, England

KLABU ya Crystal Palace juzi usiku ilikamilisha usajili wa beki wa kati, Mamadou Sakho.

Sakho wa Liverpool, aliwahi kucheza Palace kwa mkopo na dili la juzi linatajwa kuigharimu timu hiyo kitita cha pauni milioni 26.

Mahrez alikoroga kubaki Leicester

LONDON, England

NYOTA Riyad Mahrez, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushindikana kwa mpango wake wa kuondoka Leicester City.

Mabosi wake hao wamekerwa na kitendo chake cha kuwasumbua, aking’ang’ania kuondoka kwa kipindi chote cha usajili.

Mbappe achekelea kumalizana na PSG

PARIS, Ufaramsa

STRAIKA chipukizi, Kylian Mbappe, amefurahia usajili wake PSG, akiahidi kujifunza mengi klabuni hapo.

Mfaransa huyo amejiunga na PSG kwa mkopo wa muda mrefu akitokea kwa mabingwa wa Ligue 1 msimu uliopita, Monaco.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU