CHAMBERLAIN ACHEKELEA KUTUA LIVERPOOL, KLOPP AKUMBUSHIA BALAA LAKE

CHAMBERLAIN ACHEKELEA KUTUA LIVERPOOL, KLOPP AKUMBUSHIA BALAA LAKE

597
0
KUSHIRIKI
LONDON, ENGLAND - FEBRUARY 11: Alex Oxlade-Chamberlain of Arsenal during the Premier League match between Arsenal and Hull City at Emirates Stadium on February 11, 2017 in London, England. (Photo by Catherine Ivill - AMA/Getty Images)

MERSEYSIDE, Liverpool

BAADA ya kukamilisha dili la uhamisho wake wa kutua katika klabu ya Liverpool akitokea Arsenal, kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, ameonesha wazi furaha yake ya kutinga uzi wa majogoo hao msimu huu.

Chamberlain alitangazwa rasmi kuwa mchezaji halali wa Liverpool jana mchana, baada ya klabu hiyo kukubali kulipa pauni milioni 35 za uhamisho wake, akisaini mkataba wa miaka mitano ambapo atalipwa mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki.

“Nimefurahi kutua Liverpool na niwashukuru waliofanikisha hili dili kukamilika.

“Nafahamu nimewashtua wengi kwa kuichagua Liverpool na uamuzi wa kuondoka pia ulikuwa mgumu kwani nimeishi Arsenal kwa muda mrefu, lakini naona kuhama kwangu ni kwa ajili ya manufaa ya maisha yangu ya soka,” alisema.

Naye kocha wa klabu hiyo ya Liverpool, Jurgen Klopp, alinukuliwa akisema dili la Chamberlain limemfurahisha na alilisubiri kwa hamu baada ya kuichapa Arsenal mabao 4-0 wikiendi iliyopita.

“Amefanya uamuzi mgumu sana kuiacha klabu kubwa na kuja kwenye klabu kubwa. Ni mchezaji mzuri na mwenye moyo wa kujituma. Nakumbuka mara ya kwanza nilimwona Arsenal ilicheza na Dortmund na alipoingia kutokea benchi aliubadili mchezo mzima.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU