MAJANGA HAYA HAYATAWAACHA BARCA SALAMA

MAJANGA HAYA HAYATAWAACHA BARCA SALAMA

429
0
KUSHIRIKI

CATALONIA, Hispania

DIRISHA la usajili wa majira haya ya kiangazi limekuwa chungu sana kwa klabu ya Barcelona na pigo kubwa zaidi ni jinsi ilivyoshindikana kusajili staa yeyote katika siku ya mwisho ya usajili.

Kwa muda wote wa dirisha la usajili, Barca ilikuwa ikikiona cha moto kwa wachezaji ambao walikuwa wakiwatamani na kama hiyo haitoshi wakashuhudia Neymar akisepa zake PSG bila kutarajiwa.

Ni nini kilichowakumba Blaugrana? Hebu tazama haya majanga 11 ambayo hayakuwaacha salama kabisa.

 

Neymar

Barca hawatakuja kusahau jinsi Neymar alivyowakimbia na kwenda kuvunja rekodi ya dunia ya uhamisho kwa kutua Ufaransa.

Maana yake ni kwamba, uendeshaji wa klabu ya Barca umekuwa mbovu, hakuna kigogo yeyote aliyeonesha kujaribu kuzuia hilo lisitokee hadi ilipokuja kutokea wameshachelewa.

Ila sio mbaya kiuchumi wamenufaika, euro milioni 222 si haba lakini kidonda walichobaki nacho ni kikubwa.

 

Sekeseke la Verratti

Kiungo Marco Verratti, alikuwa ni staa wa kwanza kabisa kufukuziwa na Barca kiasi cha Mwitaliano huyo kuipa presha PSG imruhusu asepe.

Hata hivyo, Barca ilishindwa kukamilisha dili licha ya kwamba rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu, aliingilia muziki na kutaka kuhitimisha mambo.

 

Msimamo wa Liverpool

Kwa mara nyingine, matumaini ya Barca kuwa Liverpool ingekubali kumwachia kiungo wao Mbrazil, Philippe Coutinho, yalikuwa si sahihi.

Walijaribu hata kuweka ofa nono mezani ya euro milioni 150 lakini ikashindikana kabisa. Doh!

 

Ishu ya kushtusha ya Seri

Ingawa Barcelona walishakubaliana mambo binafsi ya kiungo Jean Michael Seri na kupeleka wawakilishi wao katika klabu ya Nice ili kukamilisha dili hilo, walikuja kuzima mpango huo saa chache baadaye kwa kilichodaiwa kuwa Barca ilishindwa kuelewa thamani ya kweli ya kuuvunja mkataba wake!

 

Kutorudi kwa Bellerin

Ishu hii ni kama ya Verratti na Coutinho, Barcelona pia walitaka Hector Bellerin kuisaliti klabu yake ya Arsenal na kuwalazimisha wamuuze, lakini staa huyo hakufanya hivyo na Arsene Wenger hakuwa na nia ya kumwachia.

Barcelona baadaye wakaja na utetezi wa ‘kitoto’, eti hawakumtaka staa huyo na hawana sera ya kusajili wachezaji wao wa zamani.

 

Pep Segura

Katika hali ya kushangaza, siku chache baada ya dirisha la usajili kufunguliwa, Bartomeu alimtangaza Pep Segura kuwa mkuu wa kushughulika na masuala ya usajili, juu ya Robert Fernandez.

Kitendo hicho cha wakurugenzi wa michezo kikageuka kuwa Mnara wa Babeli, kila mtu akawa anaongea lake.

 

Wafuata mkumbo

Ingawa Barcelona ilikuwa haijawahi kuonesha nia ya kumsajili kiungo wa zamani wa Real Betis, Dani Ceballos, walikuja kuibuka ghafla kudai wanamhitaji waliposikia Real Madrid wanakaribia kumnyakua.

Barca ilitaka kuwaharibia Madrid kwa kutaja ofa nono lakini ilishindikana na Ceballos akaenda zake Madrid.

 

Wasioelewa la kufanya

Mwanzoni Barca ilidaiwa kumfukuzia straika wa Juventus, Paulo Dybala, lakini walipoona hawawezi kumsajili Coutinho, wakaifuata Juve siku moja kabla dirisha halijafungwa wakidhani watafanikiwa, Juve wakagoma.

 

Turan kadoda

Barcelona ilitamani sana kuona garasa lao, Arda Turan, likiondoka katika dirisha la usajili wa majira haya ya kiangazi, lakini timu zilizokuja kumtaka ni chache na hazikuja na ofa ya maana.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU