ZIFAHAM KLABU ZILIZOVUNJA REKODI SOKO LA USAJILI

ZIFAHAM KLABU ZILIZOVUNJA REKODI SOKO LA USAJILI

378
0
KUSHIRIKI

 

LONDON, England

KIPINDI cha majira ya kiangazi mwaka huu kimetuonesha jinsi gani mchezo wa soka ulivyoingia kwenye zama mpya kabisa za usajili wa wachezaji baada ya Neymar kuwa nyota ghali duniani aliyesajiliwa kwa kiasi cha fedha chenye tarakimu tatu (100+) kabla Ousmane Dembele na Kylian Mbappe hawajafuatia.

Wakati kukiwa hamna timu yoyote ya Ligi Kuu England iliyofanya usajili wa kuvunja rekodi ya dunia, bado ligi hiyo ilifanikiwa kukamata nafasi ya kwanza duniani kwa klabu zake kutumia jumla ya pauni bilioni 1.4.

Cha kushangaza zaidi, timu 14 kati ya 20 ziliandika rekodi zao mpya za usajili huku nne zikivunja rekodi hizo kwa zaidi ya mara moja.

Mtandao wa Daily Mail uliorodhesha baadhi ya timu hizo zilivyovunja rekodi zao binafsi na wachezaji gani waliochukua viti vya ufalme katika timu hizo.

 

Chelsea: Alvaro Morata – Pauni mil. 70.6

Ya zamani: Fernando Torres – Pauni milioni 50 (2011).

Licha ya kushindwa kumuuza kabisa straika Diego Costa, kocha wa Chelsea huenda akawa na faraja zaidi kwa kumpata mrithi wa nafasi yake, Alvaro Morata kutoka Real Madrid.

Morata, straika wa Kihispania, amefanikiwa kuanza kuonesha makeke yake na hata kumpiku Torres ambaye alikuja kuifungia Chelsea bao la kwanza baada ya mechi 14 na dakika 903.

 

Liverpool: Naby Keita – Pauni mil. 55

Ya zamani: Mohamed Salah – Pauni milioni 39 (2017).

Liverpool walifanikiwa kuwa moja ya timu nne zilizovunja rekodi binafsi ya kununua mchezaji kwa zaidi ya mara moja katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi msimu huu, kwani baada ya Salah kuvunja ile ya Andy Carroll ya pauni milioni 35 (2011), Keita naye akaivunja rekodi ya Farao huyo baada ya Liver kukubaliana na RB Leipzig kuhusu uhamisho wa kiungo huyo atakayetua Anfield Januari mwakani.

 

Arsenal: Alexandre Lacazette – Pauni mil. 53

Ya zamani: Mesut Ozil – Pauni milioni 42 (2013)

Licha ya mashabiki wa klabu ya Arsenal kuwa katika tafrani juu ya mwenendo wa timu yao, angalau kocha Arsene Wenger alifanya kitu kizuri katika dirisha la usajili.

Wenger alifanikiwa kumnasa straika Lacazette kwa kitita kinono ambacho kiliifanya klabu yake hiyo kuvunja rekodi ya Ozil.

 

Everton: Gylfi Sigurdsson – Pauni mil. 45

Ya zamani: Jordan Pickford – Pauni milioni 30 (2017).

Katika makocha waliofanya vizuri kwenye usajili mwaka huu ni Ronald Koeman wa Everton ambaye yupo kwenye mpango wa kuacha umaarufu mkubwa England, akianza kwa kununua mastaa wenye majina, akiwemo Sigurdsson.

Gharama iliyotumika kumnasa kiungo huyo iliivunja ile ya mlinda mlango, Pickford ambaye naye alivunja rekodi ya Romelu Lukaku ya kusajiliwa kwa pauni milioni 28 mwaka 2014.

 

Tottenham: Davison Sanchez – Pauni mil. 42

Ya zamani: Moussa Sissoko na Erik Lamela – Pauni milioni 30 (2016, 2013).

Kocha wa klabu hiyo, Mauricio Pochettino, alionekana kama amelala wakati wenzake wakihangaika huku na huko kusaka wachezaji, lakini baada ya muda mrefu akamsajili mmoja wa mabeki chipukizi anayetabiriwa makubwa siku za usoni.

 

Klabu sita zilizoshindwa kuvunja rekodi zao

Manchester United

Paul Pogba – Pauni mil. 89 (2016)

Manchester City

Kevin De Bruyne – Pauni mil. 54 (2015)

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU