KISA CHA YAMOTO BAND KUVUNJIKA KIMYA KIMYA

KISA CHA YAMOTO BAND KUVUNJIKA KIMYA KIMYA

1387
0
KUSHIRIKI

NA TIMA SIKILO

WASANII wa Yamoto Band wamekuwa wakijitetea na kusisitiza kwamba kundi lao halijavunjika na bado wako pamoja, lakini kuna dalili za wazi zinaonyesha kwamba Yamoto Band imevunjika kimya kimya na ndio maana kila mmoja ameendelea kutoa kazi zake binafsi.

Mpaka sasa waimbaji wa bendi hiyo kama Enock Bella na Bela Flavor wameshatoa nyimbo zao kila mmoja, huku Aslay akionekana kutoa hasira zake zaidi kwa kutoa nyimbo nyingi zaidi ya wazake ambapo hadi sasa amekwishaachia takribani sita.

Wakati waimbaji hao watatu wakiachia nyimbo zao, mwenzao Marombosso hajaachia wimbo hata mmoja, lakini kumekuwa na tetesi kwamba amejiunga na lebo ya Wasafi na amekwishaonekana kwenye wimbo mmoja wa lebo hiyo uitwao Zilipendwa.

Mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi tofauti kuhusiana na bendi hiyo kuvunjika, ambapo kuna wanaodai kwamba kuvunjika kwa kundi hilo kunatokana na uvumi unaohusisha ugomvi uliotokea kwenye nyumba wanaoishi Tabata Kimanga kati ya Marombosso na mwanamke aliyezaa na Aslay.

Baada ya ugomvi huo inadaiwa kwamba, Aslay aliamua kuhama kwenye nyumba hiyo waliokuwa wanaishi pamoja na kwenda kuishi Kijichi, kisha kuamua kutoa nyimbo zake mwenyewe bila ya kumshirikisha mtu yeyote, kabla ya Beka na yeye atoe wimbo wake.

BINGWA liliamua kufuatilia ni nini kimeisibu Yamoto Band na kugundua siri kubwa iliyoifanya bendi hiyo kuvunjika kimya kimya na wao wakishindwa kuiweka wazi.

Msanii wa kwanza kuhojiwa na BINGWA kuhusiana na kisa cha bendi hiyo kuvunjika kimya kimya ni Beka Flavor, ambaye jina lake halisi ni Bakari Katuti. BINGWA lilimfuata msanii huyo na kumkuta nyumbani wanakoishi wasanii hao watatu Tabata Savanna, ambao ni yeye Enock Bella na Marombosso baada ya Aslay kuondoka.

Kama kawaida yao, Beka alianza kwa kukanusha kwamba kundi hilo halijavunjika na kusema kwamba hakuna aliyepigana kama ilivyodaiwa kwamba Marombosso alizipiga na Aslay, ambaye mpenzi wake alifokewa na msanii huyo.

Beka anasema kwamba ni kweli kulikuwa na mgogoro ambao haukuwa mkubwa kama inavyotangazwa, mgogoro huo ulikuwa katika kueleweshana, maana baada ya Yamoto Band tuliporudi kutoka Europe Coke Stiudio, tulijiona tayari tumeshakuwa watu wazima na kuomba ungozi wetu tuhame  pale Temeke  kwenye kituo, maana sisi kidogo tumeshajiweza na kituo tayari kilishakuwa na watoto wengi achilia mbali ambao wanaokuja kufanya mazoezi na kurudi nyumbani kwao.

Hivyo tuliahidi kwamba tutaishi wanne kama tulivyo na uongozi ulitukubalia ombi letu, basi tukahamia maeneo ya Tabata Kimanga (Savanna), hiyo nyumba kodi yake kwa mwezi ilikuwa ni milioni moja, tulilipia milioni sita kwa miezi sita. Nyumba hiyo ilikuwa na vyumba vinne, hivyo kila mmoja alikuwa na chumba chake na kila mtu alikuwa anafanya anachojiskia kwa kuwa hatukuwekeana masharti yoyote. Mwenzetu Aslay alimchukua mpenzi wake ambaye amezaa naye mtoto na kuishi nao pale, hivyo si unajua nyumba ikiwa na mwanamke. Kuna vitu vidogo alivifanya mzazi mwenzake au mke wa Aslay, Marombosso alikwenda nyumbani na msichana mwingine yeye akaamua kumpigia simu mpenzi wa Marombosso na kumwambia tukio hilo.

Jambo hilo lilimkwaza Marombosso ambaye alimwita shemeji yake na kumweleza ukweli, kifupi halikuwa tatizo kubwa, ila Aslay alipofikishiwa hizo taarifa na mkewe alizipokea vibaya

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU