MESSI, RONALDO WAKITELEZA TU KANE KAPETA

MESSI, RONALDO WAKITELEZA TU KANE KAPETA

517
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

KWA sasa katika ulimwengu wa soka kuna wachezaji wawili ambao wanautikisa ulimwengu kwa kupata mafanikio ya hali ya juu wakiwa na klabu zao na hata timu za mataifa wanayotoka.

 

Nyota hao ni mastraika Cristiano Ronaldo ambaye anaichezea Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno na Lionel Messi wa Barcelona, ambaye pia ni nahodha wa timu ya Argentina.

 

Kwa sasa mastaa hao kwa jina jingine unaweza kusema ndio roho ya timu za taifa na klabu zao kutokana na kuwa tegemeo kwa kila kitu, ikiwamo kuzipachikia mabao.

Mbali na hilo, pia vinara hao wawili ndio wamekuwa wakikabana koo katika kunyakua tuzo mbalimbali Ulaya na za dunia.

 

Hata hivyo, kwa sasa kuna nyota ambaye hategemewi na wengi kama anaweza kuwafunika vigogo hao, lakini anaweza kufanya hivyo, jambo ambalo litawashangaza wengi.

Staa huyo ni Harry Kane, ambaye kwa sasa anakuja kwa kasi ya ajabu, ambayo pengine mastaa hao hata wakimfunika kwa kubeba tuzo, lakini anaweza kuwafunika katika kipengele cha kucheka na nyavu.

Hadi sasa Kane ameshafunga mabao matano katika mechi tatu zilizopita wakati akiichezea  England na akiwa na umri wa miaka 24 ameshafunga mabao  125 akiwa na timu yake ya Tottenham na nchi yake, wakati  Messi alifunga 203 na Ronaldo  137 wakati wakiwa na umri kama huo.

Rekodi hiyo ndiyo pia ilimfanya kocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate, kusema wazi kwamba, Kane tayari ameshawasha moto kuwafukuzia vinara hao na huku akisema kuwa, hata iwe roho mbaya ya Kocha wa Hispania, Julen Lopetegui.

“Nilikuwa na mwingiliano fulani na Julen Lopetegui kwenye mchezo ambapo alikuwa akizungumzia jinsi nilivyokuwa na bahati ya kuwa na Harry anavyocheza. Yeye yupo kwenye kiwango cha hali ya juu, lakini pia ana mawazo ya kutaka kuwa mchezaji bora,” anasema  Southgate.

 

“Leo (juzi) asubuhi alikuwa anafahamu idadi ya mabao atakayofunga kwenye mchezo na vilevile idadi ambayo Ronaldo na Messi wanayo kwa sasa. Anapigania kuwa mchezaji bora. Na kwa nini isiwe hivyo?”anahoji kocha huyo.

 

Anasema kuwa, anamwamini mno staa huyo kutokana na kuwa amewahi kufanya kazi naye kitambo tangu akiwa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 2 na kwamba atamtumia kadri iwezekanavyo.

Anasema ni lazima amzungumzie nyota wake huyo kutokana na kuwa bado ana umri wa miaka 24, hivyo bado kuna mambo mengi yatakuja kutoka kwa straika huyo.

 

“Alan Shearer alikuwa na umri kati ya miaka 25/26 wakati alipokuwa mfungaji bora miaka  ’96. Harry bado yupo hatua za mwanzo katika kibarua chake, lakini ufungaji bora wa ligi katika kipindi cha miaka miwili unapatikana kwa haraka, hivyo Harry ana nafasi kubwa ya kufikia huko,” anasema kocha huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU