DANSA WCB ACHEKELEA MAFANIKIO

DANSA WCB ACHEKELEA MAFANIKIO

706
0
KUSHIRIKI

NA CHENGE MOHAMED (TUDARCO)

DANSA kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na msanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Plutnumz’, Emmanuel Kiyeli ‘Imma Platnumz’,  amesema anafurahi kupata mafanikio ya maonyesho ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Imma Platnumz alisema kuanzia mwaka juzi mpaka sasa wamekuwa wakipata maonyesho makubwa yanayofanya watambulike kimataifa na kujiingizia kipata kizuri.

“Nikiwa miongoni mwa madansa maarufu hapa nchini, nimekuwa nikipata kipato kikubwa kutokana na ziara zetu za kimuziki tunazoendelea kuzifanya, kwa sasa malipo ni mazuri na yanatufanya tuzidi kunufaika miongoni mwetu na pia nimeweza kumudu masomo yangu ya chuo na majukumu mengine ya kazi,” alisema Imma Platnumz.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU