GIGY MONEY AOGOPA KUCHORA TATTOO YA MPENZI WAKE

GIGY MONEY AOGOPA KUCHORA TATTOO YA MPENZI WAKE

468
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE

VIDEO VIXEN na msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa Papa, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amesema hawezi kuchora tattoo yenye jina la mpenzi wake kwani anaogopa kupata ugonjwa siku watakapoachana.

Gigy ameliambia Papaso la Burudani kuwa, anatamani kuchora ‘tattoo’ ya mpenzi wake wa sasa lakini anashindwa kuchora kwa sababu anajua atapata presha siku ambayo watakuja kuachana.

“Si kama sitamani kuchora tattoo ya nimpendaye ila mapenzi hayana ‘formula’ wala mjanja, tukiachana naweza kufa kwa presha au nikapata ugonjwa usiojulikana kwa kuwa nikifikiria gharama na jinsi nilivyoumia wakati wa kuchora ndiyo maana sitaki kabisa,” alisema Gigy Money.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU