NILISHAKUFA

NILISHAKUFA

661
0
KUSHIRIKI

Ilipoishia

B

Ilipoishia

Baada ya kufikiana kiasi hicho cha pesa ambacho toka naingia katika mji huo sijawahi kukitumia kwa usafiri wa safari moja, dereva alianzisha uchokozi.

 “Ndugu yangu naona unataka kumchukua yule mrembo,” aliongea dereva.

 “Kawaida, nampenda sana yule msichana.”

 “Utamuweza?” Dereva aliuliza.

 “Kwanini umeniuliza hivyo?”

 “Mrembo yule ananukia pesa muda wote. Watu wengi wamemshindwa.”

 “Kivipi, kwani unamfahamu?”

SASA ENDELEA

“Ni mtu gani anayekesha klabu ya Freesize au nje asimjue msichana yule? Wengi tunamjua, ni msichana ambaye kama huna pesa kumteka kirahisi rahisi ni ngumu sana labda uwe na kipaji cha mapenzi,” aliongea dereva.

“Unadhani nitashindwa?” Nilimuuliza dereva.

“Kwa mtindo wako wa kubembeleza bei ya tax, shilingi 400 unaiona kubwa sidhani kama utamuweza.

“Kwanini nishindwe bwana, mimi mwanamume. Halafu kwangu pesa si silaha kubwa sana ya kumteka mwanamke.”

“Unajua vijana wengi wa mji huu wote wanampenda Paulina, isipokuwa wanashindwa kuwa naye kwa sababu mbalimbali. Mojawapo ni kuogopa wanaume matajiri, ambao wanamsaka Paulina. Pia inasemekana kuwa mrembo yule ana mikakati ya siri ya kutafuta pesa. Hivyo mimi nakuona jasiri sana kutaka kuwa na msichana yule,” aliongea dereva maneno ambayo hayakutofautiana na maneno aliyokuwa akiniambia rafiki yangu Halid.

Sikutaka tena kumjibu dereva lolote, nilikaa kimya nikijua maneno yake yalikuwa na nguvu ya kunikatisha tamaa, japo niliyaogopa. Maana tayari moyo wangu ulikuwa na kiburi, hukutaka kabisa kuelewa jambo lolote, linalizozungumzwa kuhusu Paulina.

Baada ya dakika chache tulifika nyumbani kwangu. Ambapo niliingia ndani kuchukua shilingi 50 ambazo niliziongeza kwenye ile 300 iliyobaki na kumlipa dereva tax. Dereva alipoondoka niliingia ndani na kurukaruka kwa furaha.

Furaha yangu ilikuwa ni jinsi nilivyofanikiwa kumteka Paulina kwa muda mfupi, tofauti na mategemeo yangu ya awali. Niliona kumteka mrembo kama yule, ilikuwa ikihitaji elimu ya mapenzi ya chuo kikuu. Japo hakuwa amenikubalia ombi langu, lakini niliona kabisa baadhi ya maneno yangu,  yalikuwa yamefanikiwa kumsogeza Paulina karibu yangu.

Nilijitupa kitandani huku nikitabasamu muda wote. Hisia zangu zilinipeleka mbali sana. Zikinionesha raha ya mapenzi nitakayokuwa naipata endapo nitakuwa na Paulina. Nililikumbuka paja lake pindi tulipokuwa kwenye gari. Hakika nilizidi kuwa mwendawazimu kichaa dhidi ya mrembo Paulina.

Baadaye kidogo usingizi ulinipitia ambapo nilikuja kushtuka asubuhi ya saa 12. Niliamka upesi maana saa 1:00 ilitakiwa niwepo kazini. Baada ya kujiandaa nilielekea kabatini kuchukua pesa ambapo nilikuta nimebakiwa na kiasi cha shilingi 200 na senti tano. Nilichanganyikiwa kidogo maana pesa hiyo ilikuwa haitoshi kunisogeza kwa siku sita ambapo mshahara wangu ungetoka.

Wakati huo ndani kwangu nilikuwa nimeishiwa na baadhi ya mahitaji, kama vile, mafuta ya kupikia, unga na vinywaji. Huku nikiwa nadaiwa pesa ya umeme. Pia nikihitaji nauli ya kwenda kazini na kurudi ambayo kwa siku sita ilikuwa ni shilingi 150.

Upande fulani wa nafsi yangu ulijilaumu, kwa kile kitendo changu cha kumlipia Paulina nauli ya tax. Lakini upande mwingine wa nafsi hiyo hiyo, uliona sawa kwa kuwa mwili wangu ulishajitoa kwa Paulina kwa kila kitu.

Nilichukua shilingi 100 na kuondoka pale nyumbani. Nilipanda magari ya dakatwende na kuelekea kazini. Niliendelea kufanya kazi kwa moyo na kwa bidii.

Jioni ilipofika, nilirudi nyumbani. Siku hiyo nilipika ugali na dagaa. Tofauti na siku zote, maana sikuwa na pesa. Nikiwa naunga mboga, Halid alikuja pale nyumbani.

“Karibu besti,” nilimkaribisha.

“Kwanza kabla ya kujibu salamu yako, niambie sababu iliyokufanya unikimbie jana na kuniacha peke yangu klabu. Unajua umenitesa sana. Nimezunguka klabu yote kukutafuta,” aliongea Halid kwa hasira kidogo.

Ili kuzishusha hasira zake nilitabasamu kwanza na kumjibu.

“Nisamehe ndugu yangu sikuwa na jinsi.”

“Nipe maelezo ya kutosha wewe si wakunifanyia vile. Kama ulitekwa na majambazi niambie.”

“Hapana Halid hakukuwa na hatari yoyote ile.”

“Sasa kwanini urudi nyumbani peke yako, si tulienda wote?”

“Niliondoka na Paulina.

“Niniiiii!?” Halid alishtuka.

“Ndio hivyo, sikutaka Paulina ajue kuwa naondoka na yeye, halafu nakuacha wewe.”

“Usinitanie uliwezaje kuondoka na Paulina. Una ubavu wa kuondoka na mrembo kama yule.”

“Kwa hiyo unanidharau?”

“Sikudharau ila naangalia hali halisi. Wewe si nilikuacha unalia lia pale ukaniambia Paulina kakukataa?”

“Ngoja nikwambie besti. Nilikwambia nitafanya niwezalo ili nimpate Paulina. Baada ya wewe kuondoka pale mezani nilirudi tena na kuongea naye. Ingawa hakunikubalia niwe wake lakini alionyesha kukubali mimi kuwa karibu yake. Baadaye niliomba kumsikindikiza. Alinikubalia, tukaondoka wote. Nikamsindikiza hadi nyumbani kwao.”

Halid aliposikia hivyo hakuamini mara moja aliona kama nilikuwa namdanganya.

“Nitaamini vipi kama si unataka kujipa misifa isiyo ya kweli. Wewe ufanikiwe kumnasa Paulina kirahisi hivyo, hataa! Tunadanganyana,” aliongea Halid.

“Uongo hauna faida. Siwezi kukuongopea wewe ni ndugu yangu. Hivyo kila kitu nachokwambia ni cha kweli, Paulina alinielewa, japo alizidi kupinga mimi kuwa wake. Lakini naamini nitampata tu,” nilimjibu.

“Ulifika hadi nyumbani kwake?”

“Ndio lakini sikuingia ndani.”

“Kwa hiyo ina maana hakai na yule mwanaume wake katika nyumba hiyo?”

“Ndio anasema anaishi yeye na wadogo zake.”

“Sawa bwana inabidi niyakubali maelezo yako. Lakini sijui nikupongeze au nikulaumu,” aliongea Halid.

“Kwanini unasema hivyo?” nilimuuliza.

“Naona unazidi kujiingiza kwenye mtego wa ibilisi. Utakuja kufa kizembe,” aliongea Halid.

“Kivipi?” Nilimuuliza.

“Ninaamini kuna mambo matatu yanakuja. Jambo la kwanza huwezi kumpata Paulina. Jambo la pili ukiendelea kumfuata fuata. Kifo chako kiko mlangoni. Tatu endapo atakukubalia awe wako, basi ukubali kuwa mtumwa wake wa kumfanyia kazi na kumpelekea pesa,” aliongea Halid maneno yaliyonifanya niogope maana yalikuwa kama msamiati.

“Halid unanivunja moyo au una wivu?”

“Heeee! Niwe na wivu wa nini? Wakati mimi nina mke wangu. Na ni kweli nakuvunja moyo kwani sitaki uwe na yule mwanamke.”

“Lakini si unajua siwezi kuishi bila yeye?”

“Mmh! Hiyo ni misemo ya mapenzi tu. Kwani alikuzaa au roho yako kaishikilia yeye. Ni wewe tu unajiendekeza.”

“Nampenda na siwezi kuacha kumfuatilia,” niliongea mimi kwa kujiamini.

Halid alisimama akapiga hatua hadi kwenye kabati na kurudi. Alinitazama kwa muda mrefu na kusikitika kwa kutingisha kichwa chake. Baada ya sekunde 10 aliniuliza.

“Unampenda mama yako, dada yako na mdogo wako?”

“Wewe wajua kuwa nawapenda,” nilimjibu.

“Mimi sijui,” aliongea Halid.

“Nilishakwambia Halid kuwa familia yangu ndio kila kitu katika ulimwengu huu.”

“Sasa kama unayosema ni ya kweli, kwa nini unahangaika na yule msichana. Kama kweli unaijali familia yako, kwa nini unatafuta matatizo.”

“Matatizo yapi Halid. Mimi kuwa na Paulina hakuwezi kuiathiri familia yangu. Katika masuala ya kifedha, familia yangu ndio ya kwanza. Hata kama Paulina atahitaji pesa nitahakikisha kwanza familia yangu nimeitumia. Hivyo usije ukadhani mimi ni mjinga.”

“Hivi wewe unamjua Paulina au unamsikia? Mimi ndiye ninayemfahamu Paulina ni mwanamke hatari kwanini hutaki kuelewa ndugu yangu.”

“Hatari kivipi, ataniua au?”

“Yule anaweza akakufanya ukahama mji huu wa Wimbodone na kurudi kwenu Vensa. Pamoja na hayo unaweza ukapata matatizo mengi ambayo hukuwahi kutarajia kama utakumbana nayo,” aliongea Halid huku mishipa ya hasira ikimtoka shingoni.

“Halid mimi nimekaa na kuongea na Paulina. Nimejua kuwa Paulina ni msichana mtulivu na mtu mwema. Tabia hizo mnazompa hana kabisa. Kwanza ni mwanamke mwenye huruma na mwenye msimamo. Sema uzuri wake ndio unaomfanya ateseke kwa kufuatwa fuatwa na wanaume wengi. Hivyo ondoa shaka kuhusu mimi.”

“Fredy unadhani shetani ili akupate anakuja kwa sura ya mbwa mwitu. Hapana! Lazima atakuja kwa sura ya kondoo. Simba anapoanza kuwinda haji kwa pupa anaanza taratibu. Naomba usiwe sikio la kufa. Hebu nisikilize mimi rafiki yako, naomba uache kumfuata yule msichana,” aliongea Halid kwa hasira.

“Naomba uniamini Halid mimi nitaweza kumuoa Paulina na nitamuweka sawa.”

“Naona hutaki kunielewa, sasa mimi namfuata Paulina nakwenda kumwambia kuwa wewe una mke na watoto watatu.”

“Niniiiii! Halid unataka tugombane?”

Nini kitafuatia? Usikose kesho. 

aada ya kufikiana kiasi hicho cha pesa ambacho toka naingia katika mji huo sijawahi kukitumia kwa usafiri wa safari moja, dereva alianzisha uchokozi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU