KUMBE EVA LONGORIA HANA UJAUZITO BWANA

KUMBE EVA LONGORIA HANA UJAUZITO BWANA

308
0
KUSHIRIKI

ATHENS, Ugiriki

IMEBAINIKA kuwa prodyuza wa muvi ya ‘John Wick’ na mwigizaji aliyewahi kutesa kwenye filamu ya ‘Empire’, Eva Longoria, hana ujauzito kama wadau walivyokuwa wakidhani.

Longoria mwenye umri wa miaka 42, aliwashtusha watu kutokana na vazi alilovaa wakati akiwa nje ya nyumba huko Ugiriki aliko na mumewe, Jose ‘Pepe’ Baston.

Hii si mara ya kwanza kwa Longoria kuhusishwa na fununu za ujauzito katika miezi ya hivi karibuni.

Hata hivyo, kimwana huyo alitumia mtandao wake wa Snapchat kuwataarifu mashabiki wake kuwa hana ujauzito.

“Niliziona picha zangu, kweli naonekana kibonge,” alisikika Longoria kwenye video aliyojirekodi huku akicheka.

“Ngoja niwaambie ukweli, nilikuwa nakula sana jibini, mvinyo na keki ndio maana nimenenepa ila sina ujauzito,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU