LULU DIVA AWAZIMIKIA GHAFLA MASHABIKI ARUSHA

LULU DIVA AWAZIMIKIA GHAFLA MASHABIKI ARUSHA

467
0
KUSHIRIKI

NA GLORY MLAY

MREMBO anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Lulu Abas ‘Lulu Diva’, ameshangazwa na mashabiki wa Jiji la Arusha kwa kumpokea vyema alipotumbuiza kwa mara yake ya kwanza kwenye tamasha la Fiesta, lililofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja vya Sheik Amri Abeid.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Lulu Diva anayetamba na nyimbo kama Utamu na Nionjeshe, alisema ametokea kuwapenda ghafla mashabiki zake wa jijini humo kutokana kumpokea vyema jambo ambalo hakutegemea.

“Nilijipanga kupiga shoo kali lakini sikutarajia kama nitashangiliwa kiasi kile, nimewapenda sana Arusha kwa kuonyesha kuukubalia muziki wangu, natarajia kuendelea kufanya makubwa kwenye maonyesho mengine yanayofuata,” alisema Lulu Diva.

Wasanii wengine ambao walifanya vyema kwenye onyesho hilo ni Ali Kiba, Weusi na Nako 2 Nako, Cheen Bees, Rostam (Roma na Stamina), Vanessa Mdee, Msaga Sumu, Jux na Ben Pol.

 

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU