RAYVANNY AZINDUA COKE STUDIO DAR

RAYVANNY AZINDUA COKE STUDIO DAR

682
0
KUSHIRIKI

Na KIDAWA HASSAN (OUT)

MWIMBAJI wa Bongo Fleva kutoka ‘lebo’ ya WCB, Rayvanny, alishiriki kwenye uzinduzi wa onyesho la muziki la Coke Studio ambalo mwaka huu linafanyika kwa msimu wa tano.

Uzinduzi huo wa onyesho hilo  linalodhaminiwa na Kampuni ya kinywaji cha Coca-Cola, lilizinduliwa mwishoni mwa wiki ndani ya Club Paparazi katika Hoteli Slip Way, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na  watu mbalimbali wakiwamo wasanii; Rayvanny, Enika Afunganile ambaye alipanda stejini kushindana kuimba wakitumia midundo ya wimbo mpya wa Ali Kiba uitwao Suduce Me pamoja na wenzake kama Milazo Nickson, Juma Khalfani na Samiah Mshasha.

Akizungumza ana niaba ya wasanii wenzake, Rayvany alisema Coke Studio ni chuo cha mafunzo kwa wasanii na aliwataka Watanzania wasubiri kuona burudani kutoka ‘kolabo’ kali walizotayarisha kwa ajili ya msimu huu kwa kushirikiana na wasanii wengine wakali kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Katika msimu wa Coca Studio wasanii  wanaoshiriki wanatokea katika nchi za Kenya, Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Ivory Coast, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, DRC na Cameroon.

Kwa upande wa Tanzania wanaoshiriki msimu huu na ambao wameshafanya kolabo zao na wanamuziki kutoka nchi nyingine za Afrika ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy. Wasanii wengine kutoka nchi nyingine za Afrika ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya), Sami Dan  (Ethiopia), Bebe Cool, Eddy Kenzo, Sheebah, Ykee Benda (Uganda).

Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe (Afrika ya Kusini), Youssoupha (DR Congo), Runtown na Yemi Alade (Nigeria), Dji Tafinha (Angola), Laura Beg (Mauritius), Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi (Ghana).

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU