BABA YAKE NEYMAR ANASA PENZI LA ‘SISTADUU’

BABA YAKE NEYMAR ANASA PENZI LA ‘SISTADUU’

555
0
KUSHIRIKI

PARIS, Ufaransa

BABA mzazi wa mwanasoka Neymar, ametajwa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo, Franciely Freduzeski (38).

Taarifa za mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 kuzama kwa mlimbwende huyo, zilianza kuripotiwa na vyombo vya habari vya nchini kwao Brazil.

Mtandao wa Mundo Deportivo umenyetisha kwamba, baba huyo aliambatana na mwanadada Franciely hadi uwanjani kuitazama timu ya Taifa ya Brazil ikiiua Ecuador mabao 2-0, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani nchini Urusi.

Taarifa zimedai kwamba, wawili hao walianza kutoka tangu mzee huyo alipokuwa na mwanawe mjini Barcelona kabla ya kutimkia PSG kwa ada ya pauni milioni 198 na kuwa mchezaji ghali duniani.

Juni mwaka huu, mrembo huyo alitajwa kufika Brazil alikokwenda kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa moja kati ya miradi ya kusaidia uchangishwaji fedha kwa ajili ya kusaidia wasiojiweza, mpango ulioandaliwa na Neymar.

Hata hivyo, bado mapaparazi hawajafanikiwa kuzinasa picha za wawili hao wakiwa pamoja ingawa watu wa karibu wameshathibitisha kuwa ni wapenzi.

Franciely ambaye kabla ya taarifa hizo alikuwa singo, aliwahi kutoka na mwandishi wa habari mwenye jina kubwa nchini Brazil, Geraldo Luis. Lakini pia, aliwahi kujiachia na straika wa Flamengo, Emerson.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU