KAMUSOKO AWAPA HABARI NJEMA YANGA

KAMUSOKO AWAPA HABARI NJEMA YANGA

1616
0
KUSHIRIKI

NA ONESMO KAPINGA -NJOMBE

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Thaban Kamusoko, amesema sasa wameanza kazi ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo kuwataka mashabiki wao kutokuwa na wasiwasi.

Yanga walianza msimu mpya wa ligi hiyo kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kabla ya juzi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji ya hapa, mchezo uliopigwa Uwanja wa Sabasaba.

Baada ya matokeo hayo, Kamusoko alisema wataendelea kushinda mechi inayofuata dhidi ya Majimaji na nyinginezo.

Kiungo huyo alisema wanajiandaa vema ili kuhakikisha wanaifunga Majimaji na kuongeza pointi tatu nyingine.

Akizungumza mchezo wao na Njombe Mji, alisema ulikuwa mgumu, ingawa walishinda na kuondoka na pointi tatu tu muhimu.

Katika hatua nyingine, beki mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema haikuwa rahisi kupata ushindi dhidi ya Njombe Mji, huku akiifisia timu hiyo mpya kwenye ligi kwa ushindani ilioonyesha kwa dakika zote 90.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU