KANYE AOMBA YAISHE KWA JAY-Z

KANYE AOMBA YAISHE KWA JAY-Z

323
0
KUSHIRIKI

LAS VEGAS, Marekani

IMERIPOTIWA kuwa rapa Kanye West, ameomba kukutana na mwenzake, Jay Z, ili kuangalia uwezekano wa kumaliza tofauti zao, mtandao wa TMZ umenyetisha.

Chanzo kimoja kilichopo karibu na nyota hao kimeiambia TMZ kwamba ni Kanye ndiye anayetaka kulimaliza bifu hilo ambalo ni kama alilikoleza kwa kitendo cha kumzungumzia mke wa Jay Z, Beyonce, akiwa jukwaani.

Wiki chache zilizopita, Jay Z, aliibuka na kusema wazi Kanye amevuka mpaka kwa kuihusisha familia yake kwenye uhasama wao.

Wawili hao wamekuwa maadui kwa miaka mingi sasa, japo walikuwa marafiki wakubwa kabla ya kupata mafanikio waliyonayo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU