KISA CHA YAMOTO BAND KUVUNJIKA KIMYA KIMYA-2 MKE WA ASLAY...

KISA CHA YAMOTO BAND KUVUNJIKA KIMYA KIMYA-2 MKE WA ASLAY AWATENGANISHA

2276
0
KUSHIRIKI

NA TIMA SIKILO

WASANII wa Yamoto Band wamekuwa wakijitetea na kusisitiza kwamba kundi lao halijavunjika na bado wako pamoja, lakini kuna dalili za wazi zinaonyesha kwamba Yamoto Band imevunjika kimya kimya na ndio maana kila mmoja ameendelea kutoa kazi zake binafsi.

Mpaka sasa waimbaji wa bendi hiyo kama Enock Bella na Bela Flavor, wameshatoa nyimbo zao kila mmoja, huku Aslay akionekana kutoa hasira zake zaidi kwa kutoa nyimbo nyingi zaidi ya mwenzake ambapo hadi sasa amekwishaachia takribani 10.

lipoishia wiki iliyopita…

Jambo hilo lilimkwaza Marombosso, ambaye alimwita shemeji yake na kumweleza ukweli, kifupi halikuwa tatizo kubwa, ila Aslay alipofikishiwa hizo taarifa na mkewe alizipokea vibaya…

Endelea…

Ila baadaye wakanishirikisha maana mimi ndio mkubwa katika kundi zima na tukakaa tukaongea na baada ya mazungumzo yale tukaona tumeshakua watu wazima na tuna familia zetu, hivyo ni vyema tutengane kila mtu aishi kwa uhuru na familia yake kuliko kuendelea kuishi pamoja.

Aslay akasema yeye ataanza kutafuta nyumba, akatafuta nyumba Mbagala Kijichi na kuhama, lakini hakuondoka kwa ugomvi wala hakukuwa na tatizo lingine lolote.

Baada ya Aslay kuondoka na kwenda kuishi peke yake na familia yake mbali na wenzake wa Yamoto maisha yakaendelea, lakini baada ya muda mfupi msanii huyo akatoa wimbo wake akiwa peke yake nje ya kundi.

Baada ya wimbo huo ulioitwa Kidawa kutoka bila ya wenzake kushiriki kama ambavyo mashabiki wa bendi hiyo wamezoea, pia bila ya kuwapa taarifa kwa kuwa hawakujua lolote wala kushirikishwa na Aslay, wao walichosikia ni wimbo kuanza kupigwa kwenye vituo vya redio na kuanza kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii.

Basi wenzake baada ya kusikia hivyo kwa hofu ya wao kutoa nyimbo zao bila kuushirikisha uongozi wa Yamoto wanaweza kuonekana wakorofi wakaenda kuzungumza na Said Fella ‘Mkubwa Fella’, wakitaka kujua kinachoendelea na kuomba ruhusa na wao wapewe kibali cha kufanya kazi zao binafsi kama Aslay. Uongozi huo uliwazuia kufanya hivyo na Aslay kujitetea kwamba alikuwa anajaribisha na si kwamba amedhamiria kufanya kazi zake mwenyewe nje ya kundi lao.

Basi Beka na wenzake, Enock Bella na Marombosso wakaamua kutulia na kuendelea na mambo yao mengine, muda mfupi baadaye Aslay akatoa wimbo mwingine uitwao Angekuona pamoja na video, ambao ulibamba na unafanya vizuri hadi sasa. Jambo hilo likawashtua wenzake na kwenda tena kwa uongozi na wao kuomba wafanye kazi zao binafsi, safari hii uongozi ukawakubalia kwa sharti kwamba kila mmoja atafute meneja wake mwenyewe wa kusimamia kazi zao nje ya kundi hilo.

Ingawa wasanii hao wanadai waliagizwa kutafuta mameneja wao wa kusimamia kazi zao, lakini BINGWA lilijulishwa na watu wa karibu na bendi hiyo na uongozi kuwa Fella bado yuko nyuma ya Aslay, ingawa anayedaiwa kumsimamia msanii huyo ni meneja Yusufu Chambuso.

Baada ya wasanii wengine wa bendi hiyo ya Yamoto kuruhusiwa kufanya kazi zao, Beka alikuwa wa kwanza kutoa wimbo wake uitwao Libebe pamoja na video yake ambapo mpaka sasa bado unafanya vizuri, huku Enock Bella, akiachia wimbo wake alioupa jina la Mkuyu.

Beka anasema kuruhusiwa kutoa wimbo lilikuwa jambo zuri kwa kuwa mashabiki tulishawasikia tukifanya kazi kama kundi, ruhusa yao imetupa kibali kuonyesha uwezo wetu msanii mmoja mmoja kwani moja ya chanzo cha Aslay kutoa wimbo wake mwenyewe ni………

Itaendelea wiki ijayo

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU