MTIBWA YATAMBA KUTONG’OKA KILELENI

MTIBWA YATAMBA KUTONG’OKA KILELENI

822
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

BAADA ya kufanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila, amesema kuwa hawatakuwa tayari kuona timu yoyote inawaondoa kwenye nafasi hiyo.

Mtibwa imeifunga Mwadui 1-0 juzi na kuwa timu pekee inayoongoza ligi, huku ikiwa na pointi 6 baada ya kushinda michezo miwili mfululizo.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mtibwa ikiwa inaongozwa ligi inafuatwa na timu za Simba, Prisons, Lipuli FC, Yanga na Azam FC wenye alama nne kila mmoja.

Akizungumza na BINGWA, Katwila alisema: “Siwezi kusema timu yangu itakuwa bingwa moja kwa moja lakini haitakuwa kazi rahisi kwa timu nyingine kuniondoa kwenye nafasi hiyo.

“Hali hii itazilazimu kufanya kazi kubwa zaidi ya ninayoifanya, ili timu nyingine zisiweze kutuondoa mahali tuliopo sasa.

“Kwa sasa akili zangu ni kuhakikisha tunaendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi zetu zinazokuja, kwani hata kama hatutachukua taji basi tuwe kwenye nafasi mbili za juu mwisho wa msimu,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU