KOCHA BARCA AMVULIA KOFIA MESSI

KOCHA BARCA AMVULIA KOFIA MESSI

746
0
KUSHIRIKI

MADRID, Hispania

KWA lugha nyingine unaweza kusema ni kama anadai sio bure, baada ya kocha wa  Barcelona, Ernesto Valverde, kuweka wazi kuwa katika maisha yake hajawahi kumwona mchezaji mwenye uwezo mkubwa kama bingwa huyo mwenye tuzo tano za Ballon d’Or, Lionel Messi.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya juzi Messi kufikisha mabao 300 aliyoyafunga akiwa uwanja wa Camp Nou, baada ya kuifungia klabu yake mabao manne katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Eibar.

Katika mchezo huo, staa huyo alionesha uwezo wa hali ya juu na kuisaidia timu yake kukaa kileleni kwa pointi 15 baada ya kucheza michezo mitano, huku wapinzani wao, Real Madrid wakishika nafasi ya 5 baada na pointi nane kabla ya mchezo wa jana.

“Messi ni mchezaji wa kipekee, muda wowote anaweza kubadilisha matokeo, naweza kusema sijawahi kumwona mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu kama yeye katika maisha yangu, ana kila sababu ya kutajwa kuwa ni bora duniani.

“Nilikuwa na wasiwasi katika mchezo huo kwa kuwa Messi alicheza peke yake bila ya Luis Suarez, lakini aliweza kuonesha kuwa ana uwezo wa kubadilisha mchezo muda wowote, aliufanya mchezo huo kuwa rahisi sana, alitengeneza nafasi nyingi kwa upande wetu ambazo zilikuwa mbaya kwa wapinzani wetu.

 

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU