NEY WA MITEGO AIBUKA CHIMBO LA CHID BENZ

NEY WA MITEGO AIBUKA CHIMBO LA CHID BENZ

330
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KATIKA hali ya kuweka fumbo mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, juzi aliibuka nyumbani wa rapa Chid Benz, Ilala Boma na kuzungumza naye mengi ambayo amekataa kuyaweka wazi.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Ney aliwataka mashabiki wa muziki wake wakae tayari, kwani Oktoba kuna kitu kikubwa kinakuja japo hakutaka kufafanua kama ni wimbo au kuna tukio atakalomshirikisha Chid Benz.

“Tupige kimya kwanza hadi Oktoba 14, watu wasubiri unajua nimeamini bora uishi kama uko peke yako usimwamini hata unayedhani ni rafiki yako na ishi na kila mshkaji kwa tahadhari,” alisema Ney kwa mafumbo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU