WADAU WAZISAPOTI TIMU ZA MIKOANI

WADAU WAZISAPOTI TIMU ZA MIKOANI

254
0
KUSHIRIKI

 

LIGI Kuu Tanzania Bara  inaendelea kushika kasi tangu ilipoanza Septemba 26, huku timu 16 zikiwania ubingwa wa mismu huu.

Hata hivyo, licha ya kuwa bado ni mwanzoni kabisa, tayari kuna baadhi ya timu hususan za mikoani zimekuwa  na mwanzo ambao na hii ni ishara mbaya kama zitaweza kumudu mikikimikiki ya michuano hiyo.

Baadhi ya timu hizo ni Majimaji, Ruvu Shooting, Kagera Sugar na Stand United ambazo hadi sasa hazijaweza kupata ushindi hata mmoja katika michezo yake mitatu ama minne.

Sisi kwetu BINGWA  kufungwa  kwa timu hizo si tatizo kubwa,  pamoja na kupoteza michezo yake, lakini zimekuwa zikionesha kandanda safi.

Tunaomba wadau wa soka kuhakikisha wanazisapoti timu zao za mikoani  ili ziweze kuzinduka na hatimaye  kufanya vizuri.

Ombi letu hilo kwa wadau linatokana na kwamba  kwa kiasi kikubwa hazina udhamini mkubwa kama zilivyo Simba, Yanga, Azam FC  na hata zile zinazomilikiwa na taasisi mbalimbali.

 

Kama inavyofahamika kuendesha timu si suala dogo, ni jambo ambalo linahitaji uwekezaji mkubwa hivyo jukumu hilo pia lipo mikononi mwa wadau hao ambao wanatakiwa kuelekeza nguvu zao hata kwa timu za mikoani badala ya kuangalia zenye majina makubwa.

 

Tuna imani kama zitapata msaada huo zitaweza kufanya vizuri, kwani zinaonekana kuwa na  vikosi vizuri ambavyo vinaweza kuleta ushindani.

 

Kwa upande wa timu hizo, BINGWA tunaziomba zisikate  tamaa mapema kwani huu ndio mwanzo wa ligi, kinachotakiwa ni kutilia na kujipanga  ili kujenga morali ya timu na ushiriki mzuri wa michezo inayofuata.

Tunafahamu kwa sasa timu hizo zipo katika msongo mkubwa sana wa  kupata ushindi na zisipoangalia  mambo yatawaharibikia  katika safari ya kuwania ubingwa huo.

Hivyo wachezaji wanahitaji matibabu ya kisaikolojia  kwa maana ya kuwarudisha katika hali ya mchezo na kuwapa hali ya kujiamini kushinda na si kukamia mchezo ili kutopunguza umakini.

Endapo wachezaji wataamua kukamia, itawapunguzia  umakini wa mchezo na kuwa na papara nyingi zilizokosa utulivu na mwisho wake watapata  nafasi na watashindwa  kuzitumia.

Tunahitimisha kwa kuzitakia  ushiriki mzuri wenye  ushindani na wenye  matokeo mazuri katika michezo ijayo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU