ASLAY AMWAGA SIRI YA KUACHIA NGOMA MFULULIZO

ASLAY AMWAGA SIRI YA KUACHIA NGOMA MFULULIZO

1107
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka, jana aliachia wimbo wake mpya unaoitwa Natamba, huku akitoa siri ya kuachia nyimbo mfululizo ambazo zimempa mafanikio makubwa.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Aslay alisema aliibiwa ‘flash’ ambayo ilikuwa na nyimbo nyingi alizorekodi wakati yupo Yamoto Band, ndiyo maana akaamua kuziachia nyimbo mfululizo ili aliyemwibia asiweze kumpa hasara.

“Wakati bado nipo Yamoto hizi nyimbo zote nilikuwa tayari ninazo mkononi, nilikuwa nimeziweka kwenye ‘flash’ ambayo baadaye niliibiwa, ili nisile hasara na mimi nikaamua kumwaga mboga kwa kuzitoa kwa fujo, nashukuru kila wimbo nikiutoa watu wanaupokea vizuri,” alisema Aslay.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU