DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA MAROMBOSO KUTUA WCB

DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA MAROMBOSO KUTUA WCB

841
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kundi la Yamoto Band kuvunjika na kila msanii kuanza kufanya muziki kivyake, Bosi wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amemtangaza mwanamuziki, Mbwana Yusuph ‘Maromboso’ kuwa memba mpya wa lebo yake.

Diamond ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake mpya, Hallelujah amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram akimtakia Maromboso heri ya siku ya kuzaliwa huku akionyesha shauku kubwa kumtambulisha msanii huyo mpya wa WCB rasmi.

“Kheri ya siku ya kuzaliwa Maromboso, maneno kamwe hayataweza kutosha kuelezea ni kiasi gani mimi ni shabiki wako, heshima na busara zako hunifunza mengi, nasubiri kwa hamu siku ya utambulisho wako rasmi kama msanii na mwanafamilia wa WCB, vile vile ulimwengu kusikia kipaji kingine kizuri kutoka Tanzania,” aliandika Diamond Platnumz.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU